Mjumbe wa Baraza kuu UVCCM Viti vitatu Bara Ndg. Shamira Mshangama akiwa kwenye muendelezo wa ziara yake ya kuimarisha uhai wa Jumuiya ya Vijana CCM na kuhamasisha ushiriki wa vijana kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka huu 2025.
Shamira alitembelea ofisi ya UVCCM Mkoa wa Kaskazini Unguja, Zanzibar kufanya kikao kifupi cha ndani, na kukabidhi shilingi milioni moja kwa kamati ya Utekelezaji na viongozi wa Baraza la UVCCM Mkoa wa Kaskazini Unguja iliyopokelewa na Katibu wa UVCCM Mkoa huo Comrade Rished Khalfan pamoja na wajumbe wengine ngazi ya mkoa na Wilaya.
Shamira amewasisitiza kuwa pamoja na kazi zote tunazofanya lakini viongozi tunajukumu la kuzingatia ujenzi wa CCM na Jumuiya zake.“Ujenzi wa Chama ni jukumu letu sote”.