NA WILLIUM PAUL, MOSHI.

Akitoa taarifa za ujio huo ofisini kwake kwa Waandishi wa Habari, Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu amesema kuwa, Waziri Mkuu atawasili kesho Kilimanjaro na kwenda moja kwa moja wilayani Mwanga ambapo atazindua geti la utalii lililopo kata ya Karambandea.
Amesema kuwa, geti hilo litawasaidia Watalii watakaotaka kutembelea hifadhi ya Taifa ya Mkomazi kupitia geti hilo badala ya kupita katika wilaya ya Same.
“Akiwa Mwanga ataifungua pia hospitali ya wagonjwa wa saratani ya mama ngoma na badae kuweka jiwe la msingi katika ofisi ya utalawa ya halmashauri ya Mwanga na badae kufanya mkutano wa hadhara Usangi” amesema Babu.
Mkuu huyo wa mkoa amesema kuwa, siku ya kwanza ya Waziri Mkuu itakuwa imeisha huku ratiba ya siku ya pili atakuwa katika wilaya ya Moshi ambapo atatembelea shule ya Wasichana ya Old moshi na kuzindua shule hiyo ambapo serikali ilitoa fedha kwa ajili ya kukarabati shule hiyo ambapo kwa sasa imeshapokea wanafunzi wa kidato cha tano.
Ameendelea kudai kuwa, mara baada ya uzinduzi huyo, Waziri Mkuu ataenda wilayani Rombo ambapo atatembelea barabara ya lower road ambapo barabara hii ni muhimu kwani wananchi wanaitegemea sana.
Amesema kuwa, atapewa maelezo na Meneja wa Tanroad na kuikagua barabara hiyo mpaka Tarakea ambapo kipo kipambe za mita 680 ambacho kimeshawekwa lami huku kilomita kumi zipo kwenye manunuzi na badae kufanya mkutano wa hadhara Tarakea na badae kuelekea Himo ambapo atafanya pia mkutano wa hadhara.
Mkuu huyo wa mkoa amewasihi wananchi kujitokeza kwa wingi katika maeneo ambapo patafanyika mikutano ya hadhara ili kumsikiliza pamoja na kumlaki kwa wingi.