Wafanyakazi wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) wakiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunzi wanaosoma masomo ya biashara katika Shule ya Sekondari ya Eckernford mkoani Tanga.
Mkuu wa shule ya Sekondari ya Eckernford akiwatambulisha na kuwakaribisha wafanyakazi wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) waliofika shuleni hapo kwa ajili ya kuwahamasisha wanafunzi kujiunga na masomo ya Uhasibu watakapomaliza masomo yao ya Sekondari.
Afisa Masoko na Mawasiliano Mwandamizi wa NBAA, Magreth Kageya akitoa elimu kuhusu kazi zinazofanywa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) kwa wanafunzi wanaosoma masomo ya biashara wa Shule ya Sekondari ya Eckernford iliyopo mkoani Tanga.
Mfanyakazi wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), Sawa Ngendabanka akitoa elimu kwa wanafunzi wanaosoma masomo ya biashara wa Shule ya Sekondari ya Eckernford pamoja na kuwahamasisha wanafunzi hao kujiunga na masomo ya Uhasibu watakapomaliza masomo ya Sekondari.
Baadhi ya wanafunzi wanaosoma masomo ya biashara wa Shule ya Sekondari ya Eckernford wakiuliza maswali mara baada ya kupata elimu iliyokuwa inatolewa na wafanyakazi wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) waliofika kutoa elimu shuleni hapo mkoani Tanga.
Baadhi ya wanafunzi wanaosoma masomo ya biashara na walimu wa Shule ya Sekondari ya Eckernford wakifuatilia mafunzo yaliyokuwa yanatolewa na wafanyakazi wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) waliofika kutoa elimu shuleni hapo mkoani Tanga.