Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama leo Machi 26, 2025 amewasilisha ujumbe maalum wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa Rais wa Jamhuri ya Malawi Mhe. Lazarus Chakwera katika Ikulu ya Rais iliyopo Jijini Lilongwe, Malawi.
Rais Chakwera amemshukuru Rais Samia kwa ujumbe huo maalum na kubainisha ya kuwa Malawi na Tanzania zitaendeleza ushirikiano wa kihistoria uliopo baina ya mataifa hayo mawili.
Waziri Mhagama akiwa ameambatana na Balozi wa Tanzania nchini Malawi Mhe.Agnes Kayola pamoja na ujumbe wake amemshukuru Rais Chakwera kwa mapokezi mazuri na kusema kuwa Rais Samia anashukuru na kutambua umuhimu wa kuendeleza mahusiano mazuri ya kidiplomasia kati ya Tanzania Malawi ambayo yanawanufaisha raia wa nchi zote.