imesema inatambua mchango mkubwa wa watoa huduma za kifedha nchini
katika kuwahudumia wananchi ili kuhakikisha wanapata fursa ya kufanya
miamala ya kifedha kwa urahisi, hasa katika maeneo ambayo benki
hazijafika.
yameelezwa na Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe, Mkoa wa Mwanza, Mhe.
Christopher Ngubiagai, alipokutana na Timu ya Wataalamu kutoka Wizara ya
Fedha na Taasisi zake, ambayo ipo mkoani Mwanza kutoa elimu ya fedha
kwa makundi mbalimbali.
kuwa watoa huduma za fedha wamekua na mchango katika kukuza uchumi wa
wananchi kwa kuwa kupitia watoa huduma hao wananchi wameweza kupata
mikopo, kujiwekea akiba na kufanya malipo kwa njia za kidijitali.
itaendelea kushirikiana na watoa huduma za fedha nchini ili kuhakikisha
kuwa huduma hizi zinaimarishwa na kuwafikia wananchi wengi zaidi,
hususan waliopo vijijini na maeneo ya mbali.” Alisema Mhe. Ngubiagai.
kuwa pamoja na kazi nzuri inayofanywa na watoa huduma za fedha nchini,
aliwataka kufuata sheria, kanuni na taratibu katika kutekeleza majukumu
yao ili kuhakikisha usalama wa mifumo ya kifedha, ulinzi wa watumiaji wa
huduma za kifedha na kukuza uaminifu katika sekta hiyo.
upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya
Ukerewe, Bw. Goodlucky Mtigandi, alisema mafunzo ya elimu ya fedha
yamefika wakati muafaka kipindi ambacho wanashughulikia migogoro
mbalimbali ya mikopo umiza.
mafunzo haya yatawasaidia wananchi kutambua umuhimu wa matumizi sahihi
ya fedha kwa maisha ya leo na kesho”, alisema Bw. Mtigandi.
Afisa Usimamizi wa Fedha, Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha, Wizara
ya Fedha, Bi. Elizabeth Mnzava, alizisisitiza Taasisi za Fedha zinazotoa
mikopo kwa wananchi kuhakikisha wanarudisha dhamana kwa wakopaji mara
tu wanapomaliza marejesho ya mikopo.
baada ya kupatiwa mafunzo ya fedha mmoja wa washiriki, ambaye ni
Mwenyekiti wa Chemba ya Biashara Wilaya ya Ukerewe, Bw. Baraka Jeremiah,
aliiomba Serikali kuendelea kutoa elimu ya fedha kwa mkopaji na
mkopeshaji ili pande zote mbili zijue haki, wajibu na sheria
zinazotakiwa kufuatwa.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe , mkoani Mwanza, Bw. Goodlucky Mtigandi, akikabidhiwa vipeperushi na Afisa Usimamizi wa Fedha, Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bw. Stanley Kibakaya, vyenye mada mbalimbali ikiwemo akiba, mikopo na uwekezaji ambazo zitafundishwa kwa wananchi wa Halmashauri hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe,
Mkoa wa Mwanza, Mhe. Christopher Ngubiagai, akizungumza alipokutana na
Timu ya wataalamu kutoka Wizara ya Fedha na Taasisi zake, ambao walifika
ofisini kwake kujitambulisha ili kuanza kutoa elimu ya fedha kwa
wananchi katika maeneo mbalimbali wilayani humo.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji
wa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe, Bw. Goodlucky Mtigandi, akizungumza
alipokutana na Timu ya wataalamu kutoka Wizara ya Fedha na Taasisi
zake, ambao walifika ofisini kwake kujitambulisha ili kuanza kutoa elimu
ya fedha kwa wananchi katika maeneo mbalimbali ya Halmashauri hiyo.
Afisa Usimamizi wa Fedha,
Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bi. Elizabeth
Mnzava, akigawa vipeperushi vyenye mada mbalimbali ikiwemo akiba,
uwekezaji, mikopo kwa washiriki wa mafunzo ya elimu ya fedha
yaliyotolewa na Wizara ya Fedha na Taasisi zake, wilayani Ukerewe,
Mwanza.
Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe,
Mkoa wa Mwanza, Mhe. Christopher Ngubiagai, akiwasikiliza Timu ya
wataalamu kutoka Wizara ya Fedha na Taasisi zake, ambao walifika ofisini
kwake kujitambulisha ili kuanza kutoa elimu ya fedha kwa wananchi
katika maeneo mbalimbali wilayani humo.
Afisa Sheria Mwandamizi,
Idara ya Ustawi na Huduma Jumuishi za Fedha, Benki Kuu ya Tanzania
(BoT), Bw. Ramadhani Myonga, akitoa mafunzo ya elimu ya fedha kwa wakazi
wa Nansio, wilayani Ukerewe, mkoani Mwanza, walioshiriki mafunzo ya
elimu ya fedha yaliyotolewa na Wizara ya Fedha na Taasisi zake.
Afisa Masoko Mwandamizi,
Kampuni ya Uwekezaji ya UTT – AMIS, Bw. Rahim Mwanga, akitoa mafunzo ya
elimu ya fedha kwa wakazi wa Nansio, wilayani Ukerewe, mkoani Mwanza
walioshiriki mafunzo ya elimu ya fedha yaliyotolewa na Wizara ya Fedha
na Taasisi zake.
Mmoja wa washiriki wa
mafunzo ya elimu ya fedha mkazi wa Nansio, wilayani Ukerewe, mkoani
Mwanza, Bw. Octavius Kasyololo, akiuliza swali kuhusu kiwango cha riba
wakati wa mafunzo ya elimu ya fedha yaliyotolewa na Wizara ya Fedha na
Taasisi zake.
Afisa Biashara,
Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe na Mratibu wa Huduma Ndogo za Fedha,
Bw. Mango Chacha, akitoa mafunzo ya elimu ya fedha kwa wakazi wa Nansio,
wilayani Ukerewe, mkoani Mwanza walioshiriki mafunzo ya elimu ya fedha
yaliyotolewa na Wizara ya Fedha na Taasisi zake.