Na WILLIUM PAUL, MWANGA.
MBUNGE wa viti maalum kupitia mkoa wa Kilimanjaro, Zuena Bushiri ameendelea na dhamira yake ya kuhakikisha nyumba za Makatibu wa Umoja wa Wanawake wa chama cha Mapinduzi (UWT),wilaya za mkoa wa Kilimanjaro zinakamilika ambapo amekabidhi mabati 50 kwa ajili ya nyumba hiyo wilaya ya Mwanga.
Akikabidhi mabati hayo leo, Mbunge Zuena alisema kuwa, lengo la yeye kutoa mabati hayo ni kuhakikisha nyumba hizo zinapauliwa kwa wakati na viongozi hao wanahamia na kufanya kazi zao katika mazingira rafiki.
Alisema kuwa, ameamua kurejesha anachokipata katika chama kupitia jumuiya yake ya UWT na kuahidi kuendelea kushirikiana na wanachama na viongozi mbalimbali kuhakikisha nyumba hizo zinakamilika.
Akipokea mabati hayo, Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Mwanga Amina Mrengwe alimshukuru Mbunge huyo kwa jinsi ambavyo amekuguswa kuisaidia Jumuiya hiyo na kuwaomba wadau wengine kujitokeza kusapoti ujenzi huo.
Katika makabidhiano hayo yalishuhudiwa na Katibu wa UWT wilaya ya Mwanga, Cecylia Ismail na Mjumbe wa Kamati ya utekelezaji ya UWT mkoa wa Kilimanjaro, Martina Temu.