Na Mwandishi Wetu
Shule ya Awali na Msingi Gift yenye mchepeo wa Kiingereza iliyopo Bangulo Kata ya Pugu Station, Wilaya ya Ilala, Mkoa wa Dar es Salaam imewataka wakazi wa maeneo ya Bangulo kuchangamkia fursa ya elimu itolewayo na shule hiyo kwa lengo la kupata elimu bora.
Mkurugenzi wa Shule hiyo Zawadi Kuguru anasema kwamba shule yake imejipanga kutoa elimu bora na kwa gharama nafuu kwa wakazi wa eneo hilo na kwingineko ili kujenga taifa bora la kesho.
“Nitafarijika sana iwapo wakazi wa eneo hili watachangamkia fursa ya elimu itolewayo hapa shuleni watapata elimu bora na kwa gharama nafuu,” alisema.
Anasema kuwa shule imekuwa ikipata matokeo mazuri kwa darasa la saba kwa wastani wa A nyingi na B chache na kwamba wameweza kuibua vipaji vya vijana kwa ufasaha.
“Tuna flash za nyimbo zilizorekodiwa na watoto wetu hapa, tuna wafundisha muziki kwani tunaamini katika vipaji na dunia ya sasa matajiri wengi wakubwa ni wasanii na wana michezo,” anasema.
Anabainisha kwamba shule yake itandelea kutekeleza sera mpya ya elimu kwa kuwafundisha wanafunzi kwa vitendo masomo ya Ushonaji na ufumaji ili watakapomaliza elimu zao waweze kuwa na taaluma ya kuwaongezea vipato.
Ananampongeza Rais Samia Suluhu Hassan Rais wa Sita wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuongoza nchi vizuri na kuwa Rais Mwanamke wa kupigiwa mfano barani Afrika na Duniani kote.
“Rais Samia ni Role model wangu, ananipa matumaini ya kufikia malengo yangu katika maisha na kuamini kwamba ukiwa na nia lolote linawezeka,”
Anampongeza kwa kutimiza miaka minne madarakani na kwamba kazi kubwa aliyoifanya katika kipindi chake inaonekana.