BONGOMUVI tumepata Heshima Kwa Kuendelea Kupewa sapoti ya Wadau wa tasnia ya Sanaa tusiibeze tupambane Kuhakikisha tunajiaminisha.
Akizungumza kauli hiyo Msanii wa Filamu nchini Jimmy Mafufu amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ametutoa Kimaso maso Kwa kuipa thamani Tasnia hii Kwa Kushiriki Kama Muhusika Mkuu katika Filamu ya “The Royal Tour ” hivyo ameifanya tasnia hii iheshimika.
“Mama Kuingia kwenye tasnia amekuja Kuongeza wigo mpana wa wadau Kama “StarTimes” na wengine kujitokeza na kuhakikisha wasanii tunafanya Kazi nyingi nzuri na zenye ubora ili tuwafikishie Mashabiki zetu bandika bandua”.
Hata hivyo Mafufu ameeleza ambavyo Tamthilia inayoruka StarTimes “Nice to Meet you” inavyofanya vizuri kwa sasa na ndio wakata muafaka Kama ambavyo Kampuni ya Startimes Limited Walivyotoa Ofa Kwa Mwezi Mzima kupitia Kampeni yao ya “Lipa tukubust”.
Pia ametoa pongezi kwa Startimes kwa kuendelea kutoa sapoti kwa Wasanii pamoja na kuhakikisha vifurushi vinakuwa rafiki kwa Watazamaji ili kugusa hali zote kuhakikisha wanapata burudani.
“Tunajua Mashabiki zetu ni wale watu wa hali ya chini Kabisa hivyo tunashawishika Kuwaambia kuwa Kampuni hii ni Mali salama na Mama ameweka Mazingira mazuri Kwa wawekezaji kama hawa kuendelea kuwekeza katika Tamthilia zetu za Kitanzania japo Kuna Tamthilia zingine zinazotafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili. “
Kwa upande wake Meneja wa Startimes David Malisa amesema Startimes Wamezindua kampeni hiyo ya “lipa tukubusti” ambayo ni offa ya mwezi mzima kwa wateja wake wote wa Dishi pamoja na Antenna.
“Mteja anapolipia kifurushi cha mwezi mzima basi ana bustiwa kwenda kifurushi cha juu kwa mwezi mzima bure kabisa,Lipia NYOTA mwezi – 11,000 tukubusti mpaka MAMBO – 17,000 na Vifurushi vingi hivyo hivyo.
Hata hivyo Malisa ameongeza kuwa Ofa hiyo Mahsusi Kwa Kipindi hiki cha Sikukuu ili kuweka karibu familia hususani watoto ambapo zipo katuni kwa lugha ya Kiswahili ndani ya King’amuzi cha Startimes.
Hata hivyo Hemdy Suleiman maarufu Kama Hemed PhD ameongeza kuwa Waendelee Kutazama Tamthilia hiyo ya “Nice to Meet you” kwani Kuna Mambo mengi mazuri yanakuja