
Jeshi la Polisi nchini Nigeria limefanikiwa kuwaokoa watu 21 waliotekwa nyara katika jimbo la Zamfara, huku likikamata kiasi cha Naira milioni 4.8 (sawa na shilingi milioni 15 za Kitanzania) ambazo zilikuwa ni fidia ya utekwaji. Operesheni hiyo iliyofanyika tarehe 29 Machi 2025 kwa ustadi mkubwa, imeleta matumaini kwa familia za waathiriwa na raia wa Nigeria kwa ujumla.
Kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya usalama, wahalifu hao walihusika na mfululizo wa matukio ya utekaji nyara katika eneo la mji wa Muji, ndani ya Steti ya Taraba, wakilenga raia kwa lengo la kupokea fedha za fidia. Hata hivyo, polisi waliweza kuwatia mbaroni na kuokoa mateka bila madhara makubwa.

Wakati Nigeria ikiendelea kupambana na utekaji nyara na uhalifu mwingine, ripoti mpya kutoka CEO World Magazine inaorodhesha nchi kadhaa za Kiafrika kama maeneo hatarishi zaidi kulingana na mambo kama vile vita, ugaidi, uhalifu uliopangwa, na migogoro ya silaha. Ripoti hii imeorodhesha nchi 10 hatari zaidi kutembelea barani Afrika mwaka 2025, nchi hizo ni:
- Sudan – Kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe na mgogoro wa kisiasa.
- Somalia – Kutokana na ugaidi na ukosefu wa serikali imara.
- Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) – Kutokana na mapigano ya waasi na migogoro ya kikabila.
- Jamhuri ya Afrika ya Kati – Kutokana na vita vya muda mrefu na vikundi vya waasi.
- Libya – Kutokana na mapigano kati ya makundi ya waasi na serikali.
- Mali – Kutokana na ugaidi na mapigano kati ya jeshi na waasi.
- Burkina Faso – Kutokana na ugaidi na hali mbaya ya usalama.
- Nigeria – Kutokana na ugaidi wa Boko Haram na utekaji nyara.
- Ethiopia – Kutokana na uapigano ya kikabila na changamoto za kisiasa.
- South Sudan – Kutokana na migogoro ya muda mrefu na mapigano kati ya vikundi vya kisiasa.
Ripoti hii inalenga kuwaonya wageni na wawekezaji kuhusu tahadhari wanazopaswa kuchukua wanaposafiri au kufanya biashara katika nchi hizi.