MAFANIKIO YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KATIKA KIPINDI CHA MIAKA MINNE YA SERIKALI YA AWAMU YA SITA CHINI YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NA AMIRI JESHI MKUU DKT. SAMIA SULUHU HASSAN.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya tunajivunia mafanikio makubwa tuliyoyapata katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt Samia Suluhu Hassan katika Nyanja mbalimbali ikiwemo ya rasilimali watu, vifaa na majengo, pia mafanikio katika kuzuia na kutanzua uhalifu pamoja na kuzuia na kudhibiti ajali za barabarani.
Kwa kipindi cha miaka minne, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya liliweza kupata Askari wapya 351 baada ya kumaliza mafunzo ya kijeshi katika Shule ya Polisi Tanzania – Moshi [TPS] zamani CCP. Aidha, kwa kipindi hicho jumla ya Maafisa, Wakaguzi na Askari wa vyeo mbalimbali 1,162 walipandishwa vyeo kwa ngazi mbalimbali.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya lilifanikiwa kwa kiwango kikubwa kwani tumekuwa tukitumia utaratibu wa Intelejensia na Upelelezi katika kupambana na kuzuia uhalifu na kupelekea Mkoa kuwa salama.
Kwa kipindi tajwa hapo juu, Uhalifu umepungua kwa asilimia 3 kutokana na mipango na mikakati ya kuzuia na kupambana na uhalifu ikiwemo ongezeko la rasilimali watu, vitendea kazi pamoja na matumizi mazuri ya falsafa ya Polisi Jamii na Ulinzi Shirikishi kwani wananchi wamejengewa uwezo katika kuwabaini wahalifu na katika utoaji wa taarifa za viashiria vya uhalifu.
Aidha, katika kipindi hicho, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limepata mafanikio mbalimbali katika Oparesheni, Misako na Doria ambapo watuhumiwa wa uhalifu, mali na vitu mbalimbali vya uhalifu vilipatikana na kurejeshwa kwa wahanga wa matukio ya uhalifu kama vile:-
Dawa za kulevya aina ya bhangi ilikamatwa kilogram 1,450 na gram 517 pamoja na miche 653. Watuhumiwa 342 [wanaume 329 na wanawake 13].
Dawa za kulevya aina ya Heroine uzito wa gram 19.2 ilikamatwa. Watuhumiwa 6 kati yao wanaume [wanaume 4 na wanawake 2].
Dawa za kulevya aina ya Mirungi uzito wa kilogram 3 ilikamatwa. Mtuhumiwa 1 mwanaume alikamatwa.
Pombe haramu ya moshi [gongo] ujazo wa lita 4,162 na mitambo 23 ilikamatwa. Watuhumiwa 498 walikamatwa [wanaume 312 na wanawake 186].
Silaha 40 zisizokuwa na kibali zilikamatwa kati ya hizo [Gobole 29, S/gun 29, Riffle 3 na Bastola 2].
Risasi 12 za shot gun, goroli 658 na kopo 9 zenye baruti. Watuhumiwa 42 walikamatwa.
Nyara za Serikali zenye thamani ya Tshs 1,628,970,000/= zilikamatwa. Watuhumiwa 33 walikamatwa [wanaume 29 wanawake 4].
Wahamiaji haramu 174 walaiakamtwa [Ethiopia 97, Malawi 47, Somalia 19, Burundi 6, Rwanda 5].
Bidhaa za magendo zenye thamani ya Tshs 390,580,500/= zilikamatwa pamoja na vyombo vya usafiri gari 4 na Pikipiki 6.
Noti bandi 81 za Tshs 10,000/= sawa na Tshs 810,000/= na noti 3 za Tshs 5,000/= sawa na Tshs 15,000/= jumla Tshs 825,000/= zilikamatwa. Watuhumiwa 8 wanaume walikamatwa.
Mafanikio mengine ni:-
Madini [dhahabu] yenye thamani ya Tshs 1,815,621,987.03 yaliyokuwa yametoroshwa yalikamatwa. Watuhumiwa 9 walikamatwa.
Silaha 34 zilizokuwa zimeibwa zilipatikana [Pump Action 1 na Bastola 3 pamoja na risasi 23].
Magari 5 yaliyoibwa yalipatikana [ Toyota Landcruiser Prodo 1, Howo 1, corolla 1, Toyota R4 1na Toyota IST 1].
Pikipiki 83 na Bajaji 11 zilizokuwa zimeibiwa zilipatikana maeneo Tofauti
Mali ya wizi Redio 256, mitungi ya gesi 84, majiko ya gesi 56, spika 302, TV 185, Ving’amuzi 19, mita za maji za Mamlaka ya maji safi na maji taka 16, Deck 76 na Magodoro 174 ilikamatwa.
Watuhumiwa wa mtandao wa wizi wa nishati mafuta [Petroli na Diesel] katika barabara kuu 31 walikamatwa na lita 4,250.
Watuhumiwa wa mtandao wa wizi wa mafuta katika bomba la mafuta TAZAMA PIPE LINE wapatao 12 walikamatwa na lita 1,860 pamoja na vifaa vya kutobolea bomba hilo.
Watoto 4 walioibwa [wakike 3 na kiume 1] walipatikana wakiwa hai.
Kwa upande wa mafanikio ya kesi mahakamani, Watuhumiwa 07 walipatikana na hatia ya kunyongwa hadi kufa kutokana na matukio ya mauaji.
Watuhumiwa 23 wa matukio ya kubaka na kulawiti walipatikana na hatia ya kifungo cha maisha gerezani.
Watuhumiwa 21 wa matukio ya unyang’anyi wa kutumia silaha / nguvu walipatikana na hatia ya kifungo cha jela miaka 30.
Watuhumiwa 133 wa mtandao wa wizi kwa njia ya mtandao walikamatwa.
Mlundikano wa mahabusu magerezani umepungua kwa kiwango kikubwa
Kwa upande wa usalama barabarani, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limefanikiwa kupunguza ajali za barabarani kwa asilimia 2.8 na hii imechangiwa na kupatiwa vitendea kazi vya kisasa ikiwemo Magari Mapya kwa ajili ya kufanya doria za barabara kuu [High Way Patrol], Speed Rader kwa ajili ya kupima mwendo kasi na vifaa vya kupimia ulevi kwa madereva. Pia tumeendelea kujiimarisha katika Matumizi ya mifumo ya kidigitali ya usalama barabarani ikiwemo matumizi ya POS MACHINE, VTS, TIRA MIS, RAMIS, CMIS, IRTIS na TMS kwa ajili ya kuzuia na kudhibiti makosa ya usalama barabarani na kupelekea kupungua kwa ajali za barabarani.
Aidha, kwa kipindi cha miaka minne ya Rais Samia Suluhu Hassan, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limefanikiwa kujenga vituo vya Polisi na kusogeza huduma za Kipolisi kwa Wananchi. Miongoni mwa Vituo vya Polisi vilivyojengwa Mkoa wa Mbeya ni Pamoja na:- Kituo cha Polisi Makongolosi, Kambikatoto, Itumbi, Ifumbo, Sangambi na Kituo cha Polisi Igoma.
Pia, kwa kipindi tajwa hapo juu, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limefanikiwa kupata mgao wa Magari mapya 14 kwa ajili ya kuimarisha doria na usalama ndani ya Mkoa wa Mbeya. Pia, tumefanikiwa kupata mgao wa Pikipiki 11 kwa ajili ya Wakaguzi wa Kata wanafanya kazi za Polisi Jamii hasa utoaji wa elimu ya ulinzi na usalama kwa wananachi.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshukuru Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini afande IGP CAMILLUS WAMBURA kwa kuendelea kusimamia maslahi ya Askari na Jeshi kwa ujumla na kuhakikisha Jeshi la Polisi linafanya kazi kwa Weledi, Uadilifu na Usasa kwa kutumia vifaa vya kisasa na mifumo ya kidigitali hali inayopelekea kupata matokeo chanya hasa katika kuzuia na kutanzua uhalifu.
Imetolewa na:
Kamanda wa Polisi,
Mkoa wa Mbeya.