Na Oscar Assenga, TANGA
KAMPENI ya Msaada wa kisheria ya Rais Dkt Samia Suluhu “Mama Samia Legal Aid Campaign” inatarajiwa kuanza kutoa huduma za msaada wa kisheria kwa wananchi wanaokabiliwa na migogoro mbalimbali ikiwemo ya ardhi kuanzia Aprili 8 mwaka huu mkoani Tanga huku wananchi wakihimizwa kujitokeza kwa wingi.
Msaada huo wa kisheria utaongozwa na Jopo la wataalamu zaidi ya 40 kutoka kwenye Taasisi mbalimbali za Kisheria kupitia kliniki ya utatuzi wa msaada wa sheria ya Rais Dkt Samia Suluhu.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Mkuu wa Mkoa wa Tanga Balozi,Dkt Batilda Burian alisema uwepo wa kampeni hiyo katika Mkoa Tanga utasaidia kwa kiasi kikubwa kutatua migogoro iliyopo ambayo mingine imedumu kwa muda mrefu .
Mkuu huyo wa mkoa aliwataka wananachi kuchangamkia fursa hiyo na kwamba mkoa huo utatoa ratiba maalumu ya wapi wananchi watatakiwa kwenda kwajili ya kukutana na jopo hilo la wataalamu ili kupata ufumbuzi wa migogoro yao huduma ambayo itatolewa bila gharama yeyote
Aidha alisema kampeni hiyo itazinduliwa katika viwanja vya Tangamano na itajumuisha Halmashauri zote za Mkoa wa Tanga pamoja na kwensa kwenye ngazi za chini hadi ngazi ya kata,vijiji na mitaa.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga alisema lengo la kampeni hiyo ni kuongeza uelewa wa masuala mbalimbali ya kisheria ili jamii iweze kutambua hasa katika haki za wanawake, watoto, wazee, watu wenye ulemavu na makundi yote kwa ujumla wake.
Alisema jambo la pili kwenye kampeni hiyo ni kuimarisha huduma ya ushauri wa kisheria kwa waathirika wa ukatili wa kijinsia, wengi wakiwa watoto, wakina mama na wakina baba.
Mkuu huyo wa mkoa alisema jambo la tatu ni kuongeza uelewa wa wananchi kuhusu elimu ya sheria kwa uma, masuala ya haki na wajibu pamoja na misingi mizima ya utawala bora, hiku suala la nne likiwa kutoa elimu ya usimamizi wa mirathi na masuala mazima ya urithi wa ardhi ,haki ya kumiliki mali.
“Jambo la tano ni utatuzi wa migogoro kwa viongozi wa serikali za mitaa, watendai wa kata , vijiji, wajumbe wa mabaraza ya ardhi kwa kushirikiana na wazee maalumu , machifu, viongozi wa dini na serikali, nipongeze sana timu hii nimeambiwa kwambackambi hii arusha imeweza kutatua mgogoro uliodumu kwa takribani miaka 27,”Alisema Mkuu huyo wa Mkoa.
Akizungumza wakati wa mkutano huu na waandishi wa habari Mratibu wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia Mkoa Tanga ambaye ni Afisa Uchunguzi Mkuu kutoka Wizara ya Katiba ya Sheria Laurent Burilo alisema katika maeneo mengi waliyokwisha kuyafikia changamoto kubwa zilizojitokeza ni migogoro ya ardhi ambayo imekuwa ni kilio kwenye maeneo mengi.
Aliongeza kwamba jambo jingine ni masula ya ndoa na matunzo ya watoto ikiwemo mirathi ambalo nalo limeweza kujitokeza kwenye maeneo mengi.
Akitolea mfano Burilo alisema Mikoa 23 ambayo wameifikia wamekumbana na migogoro mingi kwa mfano Mikoa 22 ambayo wameifikia wamefanikiwa kuwafikia wananchi zaidi ya milioni 2 huku wakikumbana na migogoro zaidi ya elfu ishirini kati ya migogoro hiyo migogoro zaidi ya 4000 imetatuliwa na kuisha kabisa ambapo wamekumbana na migogoro mingine ambayo imedumu kwa zaidi ya miaka kumi hadi 20