
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Queen Cuthbert Sendiga (aliyevaa miwani) akiwa pamoja wa wananchi wa Loiborsiret, Simanjiro wakati wa kuadhimisha miaka minne ya mafanikio ya Serikali ya awamu ya sita katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Na Mwandishi Wetu- Loiborsiret, Simanjiro.
Mkoa wa Manyara leo Aprili 4, 2025 umefanya tukio maalumu la kutangaza mafanikio ya Serikali ya awamu ya sita katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Maadhimisho hayo yamefanyika katika Kata ya Loiborsiret Wilayani Simanjiro, maadhimisho hayo kwa upekee yamepewa jina la “SHUKA DAY; Minne ya Mafanikio, Maendeleo kwa wote”
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Queen Cuthbert Sendiga (katikati) akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro, Bw.Fakii Raphael Lulandala (wa kwanza kushoto) pamoja na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Manyara Mhe. Peter Toima (wa kwanza kulia) wakiwa katika kuadhimisha miaka minne ya mafanikio ya Serikali ya awamu ya sita katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Akiongoza maadhimisho hayo Mkuu wa mkoa wa manyara Mhe. Queen Cuthbert Sendiga ameeleza miradi ya maendeleo iliyotekelezwa na Serikali ya awamu ya sita katika sekta mbalimbali ikiwemo Elimu, Afya, Maji, Kilimo, Madini, Mifugo, Utalii nakadhalika.
RC Sendiga ameueleza umati wa wananchi hao kwamba kwa kipindi hichi cha miaka minne Mkoa wa Manyara umepokea zaidi ya Bilioni 700 kwajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya ma ndeleo.
Aidha RC Sendiga, ameeleza umuhimu wa maadhimisho hayo kwani inatoa fursa ya kufanya tathimini ya hatua zilizopigwa na mafanikio yaliyopatikana kwenye maeneo ya mkoa kuanzia kitongoji, kijiji, Tarafa, Wilaya, Mkoa na Taifa kwa ujumala.
Mwisho kwa niaba ya wananchi RC Sendiga, ameishukuru Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwakuendelea kuwajali wananchi wa mkoa wa Manyara kwa kuridhia na kutoa fedha za miradi mbalimbali ya maendeleo Mkoani Manyara.
Sherehe hiyo ilipambwa ilikuwa moto.