Mbunge wa Jimbo la Morogoro kusini mashariki mhe,Hamis Tale Tale ametoa shilingi milioni 65 za Kitanzania lengo ikiwa ni kumalizia ofisi ya wilaya ya chama, ikiwa ni pamoja na ujenzi wa ofisi 14 Za kata .
Mhe Taletale amekabidhi Fedha hizo katika kikao Cha halmashauri kuu ya wilaya, kilicholenga kuboresha ujenzi wa ofisi za chama.
Aidha Mhe Taletale amepongeza Mhe Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassani Kwa kumuunga mkono katika shughuli za kimaedeleo katika Jimbo hilo ikiwemo uboreshaji wa miundombinu hasa barabara.maji na Afya.
Kwa upande wake mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Morogoro mhandisi Joseph Masinga amempongeza mbunge huyo kwa kuteketeza ahadi ya chama cha mapinduzi CCM