
Msanii maarufu wa sanaa ya uchekeshaji nchini Tanzania, Emmanuel Mathias almaarufu kama MC Pilipili, amejikuta katika wakati mgumu baada ya kukumbwa na maswali mazito kutoka kwa waandishi wa habari kuhusu hali ya ndoa yake.
Hali hiyo imeibuka kufuatia minong’ono inayoendelea mitandaoni na kwenye vijiwe vya burudani, ikidai kuwa ndoa ya mchekeshaji huyo huenda ikawa inapitia kipindi kigumu na “kupumulia mashine” kwa muda sasa.
Waandishi wa habari walitaka kufahamu sababu ya mchekeshaji huyo kutoonekana hadharani na mke wake kwa muda mrefu, sambamba na hatua yake ya kutoonyesha tena maisha yao ya ndoa kwenye mitandao ya kijamii kama ilivyokuwa awali.
Hata hivyo, MC Pilipili hakutoa kauli rasmi kuhusu hali hiyo, jambo ambalo limeendelea kuongeza maswali miongoni mwa mashabiki wake na wadau wa burudani.
Mashabiki wengi sasa wanasubiri kauli rasmi kutoka kwa MC Pilipili ili kufahamu ukweli kuhusu tetesi hizo na hatma ya ndoa yake.