Na Mwandishi wetu
Mzumbe Sekondari Alumni wametoa msaada wa komputa shule ya Mzumbe sekondari ikiwa ni jitahada za kuboresha teknolojia ya mawasiliano na kuboresha mbinu za kujifunza na kuendelea kusaidia ufundishaji kuwa bora zaidi.
Mwenyekiti wa Umoja wa wanafunzi waliosoma Mzumbe Sekondari (Mzumbe alumni) Edward Talawa amesema hayo wakati wa kukabidhi kompyuta hizo kwa Mkuu wa Shule ya Sekondari Mzumbe iliyopo Mkoani Morogoro.
Talawa amesema kompyuta hizo 25 zina thamani ya million 30 na zimechangwa na jumuiya ya Mzumbe Alumni ikiwa ni kuona shule inaendelea vizuri.
“Tutazidi kuboresha zaidi kwa kuleta Program (software) zitakazosaidia ufundishaji kuwa mzuri zaidi na vifaa vingine vitakavyosaidia mikutano ya moja kwa moja (Video conference),” alifafanu.
Katibu wa Alumni ya Mzumbe Collis Rutenge, amesema vitendea kazi hivu vya komputa vitafanya wanafunzi waweze kuwa bora zaidi kwa sababu kuna vitu vingi kwenye teknolojia ya habari.
“Sasa hivi dunia ni digitali tunaamini tuko sehemu nzuri kwa sababu tunafanya jitihada kubwa kufikia malengo tuliojiwekea na hivyo tunaamini vijana hawa watakuja kuwa tunu ya Taifa,” alieleza.
Awali Mjumbe wa Alumin SACP (RTD) Jamal Rwambow amehimiza wanafunzi kuwa na nidhamu ya hali ya juu ili kuweza kufikia malengo yao.
Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Mzumbe Mbaraka Kupela ameshukuru kwa msaada waliopewa na Mzumbe Alumni kwa motisha kubwa waliyotoa ambayo itasaidia sana tahasusi ya PMC.
“Tutatumia kompyuta hizi vyema ili kuhakikisha kiwango cha ufaulu kinaongezeka, hivyo wanamzumbe Alumni muendele kutusaidia ili tuzidi kutembea kifua mbele tukiamini kuna watu nyuma yetu,” alifafanua.
Wakitoa shukrani kwa Mzumbe Alumni Mwanafunzi Muljin Salumu wa kidato cha pili amesema kompyuta hizo zitawasaidia kusomea
Somo la kompyuta ni moja ya masomo kumi wanayojifunza darasani ambalo linawasaidia kujifunza vitu mbalimbali kwa njia ya nadharia na kwa njia ya vitendo.