BAADHI ya wawekezaji wa sekta ya vinywaji na chakula wameipongeza serikali kwa juhudi zake za kuendelea kuweka mazingira wezeshi ya biashara na uwekezaji nchini Kwa Kuhakikisha Nchi inakuwa salama na mifumo mizuri ya kulipa kodi kwani hatua zinazochukuliwa na serikali katika kuboresha mifumo ya kisekta, sheria, na miundombinu zinatoa fursa kwa biashara kukua na kustawi.
Haya yameelezwa leo jijini Dar es salam na Meneja Masoko wa Kampuni ya SBC Kupitia Kinywaji Pepsi Jasper Maston amesema hayo wakati akitambulisha rasmi ubia kati ya Kampuni hiyo pamoja na pizza kufanya biashara kwa pamoja na kueleza kuwa utekelezaji wa sera rafiki za biashara, serikali inasaidia kuhamasisha wawekezaji na kuleta fursa za ajira kwa wananchi, na hivyo kuchangia kwa kiasi kikubwa katika maendeleo ya uchumi wa taifa.
Aidha ameeleza kuwa Ushirikiano kati ya Pepsi na Pizza Hut ni mfano mzuri wa jinsi mazingira bora ya biashara yanavyoweza kuleta manufaa kwa sekta binafsi na kwa jamii kwa ujumla lakini pia Ubia huo utaongeza uwekezaji katika sekta ya chakula na vinywaji, huku ukitengeneza nafasi za ajira na kuleta ubunifu katika kutoa huduma bora kwa wateja,na kampeni za kuvutia zitakazotolewa na Pepsi na Pizza Hut zitachangia katika kukuza uchumi na kuongeza mashirikiano ya kibiashara.
Nae Meneja Rasilimali Sixbert Malya ameelezakuwa, ni dhahiri kuwa ushirikiano huo utaimarisha soko la biashara kwa upande wa huduma, ubora wa bidhaa, na uvumbuzi.
“hii ni fursa kwa sekta zote mbili kuimarisha uhusiano wa kibiashara na kuongeza ushindani wa soko, aidha, kupitia ubia huu, wateja wataweza kufurahia bidhaa bora na huduma za kipekee, na hivyo kuchochea soko kwa ujumla”
Hata hivyo wote kwa pamoja wamepongeza juhudi za serikali katika kubuni na kutekeleza mikakati inayowawezesha wajasiriamali na wawekezaji kupata nafasi ya kufanya biashara kwa ufanisi,Ushirikiano huu wa Pepsi na Pizza Hut ni mfano halisi wa jinsi sera bora za serikali zinavyoweza kusaidia kukuza biashara, na tunaamini kuwa hii ni hatua muhimu katika kuelekea mafanikio ya kiuchumi na maendeleo endelevu.