Leo, tarehe 9 Aprili 2025, Mbunge wa Jimbo la Madaba Dkt. Joseph Kizito Mhagama, ambaye ni Mwenyekiti wa Wabunge Wawakilishi wa umoja wa Mabunge Duniani kutoka Tanzania, amehudhuria kikao cha Kamati ya Uongozi ya Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) kilichofanyika wakati wa Mkutano wa 150 wa Umoja huo wa Mabunge, uliofanyika mjini Kashkent, Uzbekistan.
Katika mkutano huo, Mhagama amejumuika na wabunge wengine kutoka Tanzania, ambao ni Esther Matiko na Elibariki Kingu, ambao pia wameingia katika Kamati ya Uongozi ya IPU.
Kamati ya Uongozi ya IPU ni sehemu muhimu ya Umoja wa Mabunge Duniani, inayohusika na uratibu wa shughuli za kisiasa na kijamii zinazohusiana na Mabunge duniani kote, Huu ni mfano mwingine wa mchango wa Tanzania katika masuala ya kimataifa ya kisiasa na maendeleo.
Wabunge hawa watatu wa Tanzania watakuwa na jukumu la kutoa maoni na kushirikiana katika mchakato wa kuboresha ushirikiano kati ya mabunge mbalimbali duniani.