WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima, ameishukuru Benki ya Biashara ya DCB katika jitihada inazoonesha katika kuwawezesha wanawake wa kitanzania kiuchumi.
Pongezi hizo alizitoa katika hafla ya uzinduzi wa Kamati ya Kitaifa ya kuratibu masuala ya uwezeshaji wa majukwaa ya uwezeshaji wa wanawake kiuchumi.
Katika hafla hiyo iliyofanyika pamoja na zoezi la ugawaji wa nakala za vitabu vya Mwongozo wa Uandaaji na Uratibu wa Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi, Waziri Gwajima alisema majukwaa hayo muasisi wake ni Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, tangu akiwa Makamu wa Rais.
“Kamati inafanya kazi na wadau mbalimbali, sekta zote, pamoja na taasisi mbalimbali zenye jukumu la kujenga fursa za kuwawezesha wanawake kiuchumi.
“Mojawapo ni Benki ya DCB, Benki ya Biashara ya DCB ni benki yenye mipango, mikakati na fursa za kuwawezesha wajasiriamali mbalimbali kiuchumi, tukiziacha benki kama hizi katika kamati hii, tunaweza kupunguza muonekano wa fursa hizi.
Waziri Gwajina akaongeza, “Benki ya DCB tunawashukuru kwa kuwa mmoja wa wawakilishi. Nina imani kupitia ninyi, wananchi watafahamu fursa mlizonazo, na pia niwaalike wadau wengine wenye fursa za kuyajenga majukwaa yetu ya kuwawezesha wanawake kiuchumi kuungana nasi”.
Naye Mkurugenzi wa Biashara wa benki hiyo, Bw. Ramadhan Mganga, akimwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya DCB, Bw. Sabasaba Moshingi katika hafla hiyo alisema, Benki ya DCB itaendelea kuweka mkazo zaidi katika kuwawezesha wajasiriamali kiuchumi hususani wanawake, ili kuendeleza misingi imara ya kuanzishwa kwake iliyowekwa na waasisi wake miaka 22 iliyopita, ambayo ni kuwapatia mitaji wananchi wenye kipato cha chini na cha kati ili kuendeleza biashara zao zinazowasaidia kujikwamua kiuchumi.
“Benki yetu imekuwa mstari wa mbele katika kutoa mikopo kwa makundi maalumu, wakiwemo wanawake kupitia Huduma ya ‘Tausi’ Mikopo ya Bodaboda na Bajaji lakini pia tuna huduma maalumu ya mikopo kwa wafanyabiashara wa masokoni.
“Benki ya DCB kwa kuendelea kuthibitisha kuwa ni Mkombozi wa Kweli wa Maisha ya Watanzania imeendelea kubuni huduma za kiubunifu pamoja na mikopo ili kusaidia biashara za wajasiamali hususani wanawake ambapo kwa mwaka 2024 imetoa mikopo ya zaidi ya shs bilioni 100 kwa wanawake pekee.
Huduma hizi za kiubunifu nyingi zinapatikana kwa njia za kidigitali huku benki ikiendelea na mkakati wake wa uboreshaji wa ubora wa huduma na kuongezeka kwa viwango vya mikopo yake inayotolewa kwa njia za kidigitali”, aliongeza Bw. Mganga.

WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima, akionesha nakala ya mwongozo wa Uandaaji na Uratibu wa Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi, katika hafla ya uzinduzi wa Kamati ya Kitaifa ya kuratibu masuala ya uwezeshaji wa majukwaa ya uwezeshaji wa wanawake kiuchumi, jijini Dar es Salaam hivi karibuni, ambapo Benki ya Biashara DCB ilishiriki kama mmoja wa wadau muhimu katika suala zima la uwezeshaji wa wanawake kiuchumi.

Mkurugenzi wa Biashara wa Benki ya DCB, Bw. Ramadhan Mganga (kushoto), pamoja na mshiriki mwingine, akihudhuria hafla ya uzinduzi wa Kamati ya Kitaifa ya kuratibu masuala ya uwezeshaji wa majukwaa ya uwezeshaji wa wanawake kiuchumi, jijini Dar es Salaam hivi karibuni, ambapo Benki ya Biashara DCB ilishiriki kama mmoja wa wadau muhimu katika suala zima la uwezeshaji wa wanawake kiuchumi.

WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima, akihutubia katika hafla ya uzinduzi wa Kamati ya Kitaifa ya kuratibu masuala ya uwezeshaji wa majukwaa ya uwezeshaji wa wanawake kiuchumi, jijini Dar es Salaam hivi karibuni, ambapo Benki ya Biashara DCB ilishiriki kama mmoja wa wadau muhimu katika suala zima la uwezeshaji wa wanawake kiuchumi.