Waziri Dkt Dorothy Gwajima, Waziri wa Maendeleo Jamii, Jinsia , Wanawake na Makundi Maalum Atangaza Kamati Mpya ya Kuhamasisha Wanawake Kujiunga na Majukwaa ya uwezeshaji Wanawake Nchini.
Wakati Akitangaza kamati hiyo ambayo inatazamiwa kuleta Mapinduzi Makubwa hasa upande wa Wanawake na Vijana alieleza Nia ya Mhe Raisi Wa Jamhuri ya Miungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan ambaye ndiye muasisi wa majukwaa hayo toka mwaka 2016 akiwa Makamu wa Rais. Kiu yake kubwa ni Kuwajenga Wanawake uwezo, ⁸ kuwaimarisha Kiuchumi, Kimaendeleo na kuona wana shiriki katika kuwania nafasi mbali mbali za kiuongoziili na kutoa michango yao.
Kamati hiyo inategemewa kutafsiri tija ya Serikali na kutengeneza matokeo Makubwa kwa Wanawake Nchini.
Aidha kamati hii ina undwa na wataalam na wabobezi kutoka sekta mbalimbali ambao ni mahiri katika kazi zao , ni dhahiri kwamba kamati hii ya kitaifa inatarajiwa kufanya mageuzi na hamasa kubwa ili kuchochea mpango mkakati wa muongozo mpya.
Wajumbe wa kamati hiyo ni kama wafuatavyo:
1. LILIAN K MTALI-MKURUGENZI WA BIASHARA WATEJA WADOGO NA WAKATI TCB BANK- Mwenyekiti.
2. SIMON J MWAPAGATA MKURUGENZI WA-FAGDI – Makamu Mwenyekiti
3. Dr.NEEMA M OBWANA MRATIBU WA MAJUKWAA TAIFA -WMJJWM – Latibu
4. JANETH S ZOYA-MENEJA MWANDAMIZI DIRISHA LA WANAWAKE TCB BANK Katibu Msaidizi.
WAJUMBE:
5. FATMA KANGE- Mkurugenzi wa GS1 Tanzania – (Barcodes na QR Codes ) na Mtaalamu wa Viwanda Vidogo na Vya Kati (SMEs Expert)
6. FRANK SANGA-Mkuu wa Vipindi -AZAM MEDIA
7. SOPHIA MGAZA- Mtangazaji AZAM MEDIA
8. RAMADHANI MGANGA-DCB BANK
MLEZI
9. DR. JUDITH IRUNGU MHINA MKURUGENZIh WA MAKAMPUNI YA PMM ESTATE LTD
kauli mbiu ya kampeni itakayo ongozwa na kamati hii inaitwa
INUKA-IMARIKA -TUSUA- KIUCHUMI
TUTAFIKIA:
Uchumi Jumuishi Utakao Mhusisha Mwanake, Kijana katika kuelewa na kuchukua Fursa na Hatimaye kukua au Kutusua Kiuchumi.