-WANUNUZI WA MAZAO WASIOKUWA NA AKAUNTI YA BENKI YA USHIRIKA KUNYIMWA LESENI.
Na Janeth Raphael MichuziTv -Dodoma
Serikali imewataka wanunuzi wa mazao makubwa ya kimkakati,kama Korosho,Tumbaku na Mikunde kufungua akaunti katika benki ya Ushirika ambayo italenga kuhudumia wakulima na wafanyabiashara wa mazao.
Hatua hiyo imekuja,kutokana na serikali kutaka kuisaidia sekta ya kilimo,ili wakulima waweze kupata mikopo ya riba nafuu katika maenso mbalimbali hapa nchini.
Hayo yalisemwa na Waziri wa Kilimo Hussein Bashe wakati akizindua usajili wa mawakala wa benki ya Ushirika ili watu waanze kufungua akaunti katika benki hiyo.
“Ni lazima wafanyabiashara na wanunuzi wakubwa wa mazao ya Tumbaku,Korosho na mazao ya mikunde wafungue akaunti katika Benki ya Ushirika,bila kufanya hivyo hawatopewa leseni,”alisema Bashe.
Bashe amesema lengo la kuanzishwa kwa benki hiyo kutakuwa msaada mkubwa kwa wakulima hususani kwenye suala zima la uchukuaji mikipo kwa ajili ya kukuza kilimo wananchofanywa.
Waziri amesema kuwa mnunuzi yeyote wa mazao makubwa ya kibiashara hatopewa leseni ya Biashara kama hatakuwa na Akaunti ya Benki ya ushirika Tanzania.
Alifafanua zaidi ya kuwa uzinduzi rasmi wa benki hiyo utafanywa Aprili 28 na Rais Sky Samia Suluhu Hassan ili kuanza rasmi kwa benki hiyo kutoa huduma kwa jamii.
Bashe amesema kuwa haiwezekani wakulima wasifaidike na jasho lao hivyo Mfanyabiashara yeyote wa mazao makubwa hawezi kupata leseni kama hana Akaunti ya Banki hiyo ya Ushirika Tanzania.
“Naomba wafanyabiashara mkafungue akaunti ili pesa yenu izunguke kwenu nyie wenyewe lakini pia izalishe faida,”alisema Bashe.
Aidha amesema benki hiyo itakuwa msaada mkubwa sana Kwa wakulima na wafanya biashara ambao watafungua akaunti katika benki hiyo ya ushirika.
Alifafanua zaidi ya kuwa,kuanzishwa kwa benki hiyo ni maelekezo ya Rais Dkt Samia ambapo alisema lazima kuwe na Benki ya ushirika ya Taifa na mchakato huo umeshakamilika ambapo Aprili 28,2025 Dkt. Samia ataizindua Rasmi.
Naye Gabriel Jackson amesema kuanzishwa kwa Benki hiyo kutasaidia sana wakulima na wafanya biashara kwa kuchukua mikopo yenye riba nafuu ambayo itawanufaisha wap na familia zao.
Amesema serikali imekuwa mstaru wa mbele Kwa ajili ya kuwasaidia wananchi wake ndio maana inakwenda kuzindua Benki ya ushirika ambayo itakuwa kimbilio la wakulima na wafanyabiashara mbalimbali wa mazao ya chakula na biashara.