Na Janeth Raphael MichuziTv -Dodoma
Serikali Kupitia ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira imepokea taarifa kutoka sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za mitaa juu ya uhifadhi na usimamiza wa mazingira, ambapo pamoja na hayo vwamejadili changamoto na fursa zinazopatikana katika sekta hiyo.
Akizungumza Leo Jijini Dodoma wakati wa kufunga kikao kazi kilichowashirikisha maafisa mazingira kutoka Mikoa yote Tanzania Bara, Mkurugenzi wa kitengo cha ufutiliaji na tathimini ofisi ya Makamu wa Rais SIGSBERT KAVISHE amesema wameamua kuwaita maafisa hao kuja Dodoma kujadili fursa na changamoto zinazopatika katika sekta hiyo ili kuimarisha utendaji kazi.
Mkurugenzi huyo amesema ndani ya kikao kazi hicho wamefanya tathimini na kuja na maziimio kumi na moja ambapo kati yake wameona wakaimarishe biashara ya caboni, waone namna ya Kuanzisha na kuendeleza bustani za kijani pamoja na uchumi wa blue.
Awali akimkaribisha mgeni rasmi, Mkurugenzi wa mazingira KEMILEMBE MUTISA amesema pamoja na kuwaita maafisa mazingira hao, lakini jambo kubwa ambalo wamekazia ni kuwafundisha namna ya kwenda kuwaelimisha wananchi umuhimu wa usafi wa mazingira na matumizi ya nishati safi ya kupikia, ambapo wamewapa maafisa hao majiko ya nishati safi.
Akitoa neno la shukrani Afisa mazingira wa Jiji la mwanza ambaye ni mwenyekiti wa maafisa mazingira Mikoa MAGABE MNILAGO amesema anaishukuru ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na mazingira kwa kuwapa majiko na kuwajengea uwezo na kuongeza wigo mpana wa utendaji kazi hata kwa upande wa uhifadhi na usimamiza wa mazingira katika sekta hiyo.