Na Janeth Raphael MichuziTv -Dodoma
Shirika lisilo la kiserikali la Habitat Humanity of Tanzania linatarajiwa kuwanufaisha wakazi wa kijiji cha Dabalo,kilichopo Halimashauri ya Wilaya ya Chamwino, Mkoani Dodoma Kwa mradi wa ujenzi wa Makazi bora, nafuu na endelevu unaotekelezwa na katika Mikoa ya Dar es Salaam na Dodoma
Hatua hiyo imekuja baada ya shirika hilo kutembelea kijiji hicho na kujionea baadhi ya nyumba wanazoishi wakazi hao wenye hali duni ya kimaisha yakiwemo mazingira magumu wanayoishi.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo ya kutembelea vitongoji vya kijiji cha Dabalo,Mkurugenzi wa Mradi wa ujenzi wa nyumba hizo unaotekeelezwa na Habitat Humanity of Tanzania,John Masenza amesema,wanatarajia kuwafikia walengwa 2,000,ambapo kwa Dodoma katika kijiji cha Dabalo Kaya 10 Kwa walengwa ambao watakidhi vigezo vinavyostaili kujengewa nyumba .
Masenza amesema hivi sasa wako katika hatua za mwisho za kukamilisha taratibu za kumkabidhi Mkandarasi eneo ambalo litatumika kujenga nyumba hizo za gharana nafuu,ambazo watakabidhiwa wananchi waliokidhi vigezo vya kujengewa nyumba hizo.
“Tayari tumefanya zoezi la kupitia baadhi vitongoji vilivyopo ndani ya kijiji cha Dabalo,tumelifanya kwa kushirikiana na serikali ya kijiji kwa ajili ya kupata walengwa, wataoingia kwenye mpango wa kujengewa nyumba za gharama nafuu,”alisema Masenza.
xMasenza amesema wanatarajia kuanza na nyumba 10,lakini mkakati huo ni endelevu ambapo utakuwa ukifanyika katika maeneo mbalimbali hapa nchini.
Naye Mwenyekiti wa.kijiji hicho Abeid Athanas alilishkuru shirika hilo kutokana na msaada huo wa ujenzi wa nyumba za gharama nafuu Kwa walengwa wanaoishi katika mazingira magumu kwenye eneo hilo la kijiji cha Dabalo.
Amesema shirika hilo linafanya hivyo kutokana na kutokana na ushirikiano mzuri unaofanywa baina ya serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali katika maeneo nbalimbali hapa nchini kwa ya kutekeleza miradi ya maendeleo.
Amesema shirika hilo linamikakati ya kusaidia watu wanaotoka katika mazingira magumu ili kuhakikisha wanapata makazi ya kuishi,ikiwemo kumudu kujiinua kiuchumi wao na familia zao katika maeneo mbalimbali.
Kwa upande wake Nyemo Mwanjililo mkazi wa kitongoji cha Ikoyi alisema Habitat Humanity of Tanzania limefanya kazi nzuri ya kupitia walengwa ambao wanastaili kujengewa nyumba hizo.
Amesema kuna baadhi ya watu wanaishi katika mazingira magumu kutokana na hali ngumu ya kimaisha waliokuwa nayo,hivyo shirika hilo limefanya kazi kubwa ya kuwainua wakazi hao kutoka katika mazingira magumu walio nayo.