NA WILLIUM PAUL, MOSHI.
WANANCHI wa kata ya Uru Kusini katika Jimbo la Moshi vijijini mkoani Kilimanjaro wamenufaika na umaliziaji wa kituo cha Afya Uru kusini na kuondokana na adha ya muda mrefu ya kutembea umbali mrefu kutafuta huduma za kitabibu.
Kituo hicho hadi kukamilika serikali imetoa zaidi ya milioni 500 ambapo kwa sasa kunatoa huduma za kitabibu.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wameonyesha kuishukuru na kuipongeza Serikali inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na Mbunge wa Jimbo la Moshi vijijini, Prof. Patrick Ndakidemi na Diwani wa kata hiyo, Wilhad Kitali kwa jinsi ambavyo wamekuwa wakipambana kuhakikisha miradi ya maendeleo inatekelezwa katika kata hiyo.
“Tulikuwa tunatembea umbali mrefu kufuata huduma za afya lakini kukamilika kwa kituo hiki cha afya kitatusaidia sisi wananchi kutotembea umbali mrefu kufuata huduma za Afya” Alisema Zuhura Rashidi.