Na Janeth Raphael MichuziTv -Dodoma
MWANASHERIA Mkuu wa Serikali,Hamza Johari,amewataka wanachama wa chama cha Mawakili,kutumia fursa ya mkutano Mkuu kujadili changamoto mbalimbali za kisheria ikiwemo kuzifanyia kazi.
Johari amesema hayo leo jijini Dodoma,wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa chama cha mawakili wa serikali,wenye lengo wa kujadili mustakabali wa chama hiko lakini pia kujitathmini utendaji kazi wao.
“Nawapongeza kwa kuandaa Mkutano huu naomba tumieni nafasi hii kujadili changamoto zilizopo ili kuzifanyia KAZI,”amesema Johari.
Mbali na hayo amemshkuru Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali,Samwe Maneno pamoja na menejimenti nzima ya ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali,ikiwemo chama cha mawakili wa serikali,kutokana na kazi nzuri ya maandalizi ya Mkutano mkuu wa mwaka waliyofanya.
“Naupongeza uongozi wa wa chama cha Mawakili,mmeandaa vizuri mkutano huu,nimefarijika kwa sababu toka nichaguliwe ni mara yangu ya kwanza nakutana na mawakili wote nchini,”amesema Johari.
Kutokana na pongezi hizo,anasema anaamini mkutano wa 2026 utakuwa zaidi ya huu wa 2025,naimani utakuwa na sura tofauti,huku akisisitiza chama hiko kijikite kujadili mambo mbalimbali yanayohusu Chama chao na Maendelea ya sekta ya Sheria kwa ujumla.
Naye Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali amwel Maneno amesema kuna kila sababu ya kuimarisha Chama hicho cha Mawakili wa Serikali Ili kiweze kutimiza kusudi la kuanzishwa kwake na kwa kuzingatia kwamba kilianzishwa Ili kuwaleta pamoja Mawakili wa Serikali.
Amesema kada hiyo inapokuwa pamoja wanafanya majukumu yao wakiwa na imani kubwa na umoja Ili kuhakikisha kwamba Serikali inatekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Sheria
Hata hivyo Naibu Mwanasheria Mkuu huyo wa Serikali amesema wao kama mawakili watahakikisha wanatekekeza majukumu yao na kuimarisha Chama hicho Ili kiwe Chama imara kuliko Chama chochote cha kitaaluma hapa Nchini.