Tanzania imepewa heshima ya kuwa mwenyeji wa hafla ya kutangaza washindi wa Kanda ya Afrika na Bahari ya Hindi, iitwayo “Africa & Indian Ocean Gala Ceremony” itakayofanyika tarehe 28 Juni, 2025 jijini Dar es Salaam. Aidha, Bodi ya Utalii Tanzania kama Taasisi yenye jukumu la kutangaza Utalii nchini ndio itaratibu hafla hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo, Aprili 14,2025, jijini Dar-es-Salaam, Mkurugenzi Mkuu Bodi ya Utalii, Ephraim Balozi Mafuru amesema kuwa mchakato wa kupiga kura kwa kanda ya Afrika na Bahari ya Hindi ulifunguliwa rasmi tarehe 11 Machi, 2025 na utafikia tamati tarehe 4 Mei, 2025. Nchi yetu imetajwa katika vipengele zaidi ya 15 ikiwemo Nchi inayoongoza kwa Utalii Afrika (Africa’s leading Destination) – Tanzania,Bodi bora ya Utalii Afrika (Africa’s leading Tourist Board) – Bodi ya Utalii Tanzania, Kivutio Bora cha Utalii Barani Afrika (Africa’s leading Tourist Attraction) Ngorongoro, Mlima unaoongoza Afrika – Mlima Kilimanjaro
Pia amesema, Hifadhi Bora ya Taifa Barani Afrika (Africa’s leading National Park): Serengeti. Pia, Hifadhi za Kitulo, Nyerere, Udzungwa, Mahale, Arusha Tarangire na nyingine zimetajwa katika vipengele vingine kulingana na ubora wake, Uwanja Bora wa Ndege Barani Afrika – Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Bandari Bora Barani Afrika – Bandari ya Dar es Salaam, Fukwe Bora Africa: Zanzibar
“Hivyo ni baadhi tu ya vipengele ambayo vivutio vyetu vimetajwa pia kampuni za watoa huduma za usafiri, malazi na waongoza watalii nchini nazo zimetajwa katika makundi ya tuzo hizi.
Ameendelea kusema kuwa Fursa kwa Tanzania tukio hili ni kwa kuutangaza Tanzania kama kivutio bora cha utalii Duniani, kwa sababu Wageni kutoka zaidi ya nchi 30 wanatarajiwa kushiriki, wakiwemo wawekezaji, wanahabari wa kimataifa, viongozi wa sekta ya utalii na wadau mbalimbali hivyo basi kupitia jukwaa hili, tutapata nafasi ya kuonesha vivutio vyetu vya kipekee ikiwemo Milima, Hifadhi za Wanyamapori na Misitu, Fukwe, vyakula, tamaduni zetu n.k