Na Oscar Assenga, MKINGA
VIJANA waliohitimu mafunzo ya awali ya Jeshi kwa Vijana wa kujitolea Operesheni ya Miaka 60 ya Muungano katika kikosi cha Jeshi 838 KJ,Maramba wilayani Mkinga wametakiwa kuhakikisha wanajiepusha na vitendo vinavyoweza kuwasababishia matatizo ya afya ya akili na mwili.
Kauli hiyo ilitolewa na Brigedia Jenerali Hashim Komba wakati akifunga mafunzo hayo kwa kikosi cha Jeshi 838 KJ, Maramba JKT wilayani Mkinga mkoani Tanga ambaye alimwakilisha Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob Mkunda
Brigedia Komba ambaye pia ni mkuu wa operesheni na mafunzo kamanda ya Vikosi chini ya makao makuu ya Jeshi alisema kwamba baada ya vijana hao kumaliza mafunzo hayo ni muhimu kuhakikisha wanazingatia na kufuata yale yote ambayo walikuwa wanafundishwa wakati wote wa mafunzo ikiwemo kujiepusha na vitendo vinavyoweza kusababishaia matatizo ya afya ya akili na mwili ikiwemo watambue kwamba wao ni msingi wa Taifa la leo na kesho.
Aidha alisema kwamba kwa kutambua umuhimu wa vijana kwenye Taifa la Tanzania Mkuu wa Majeshi amekuwa akitoa miongozo mbalimbali ya jinsi ya kuboresha mafunzo ya vijana ili yaendane na madhumuni la kuanzishwa kwake.
“Lengo ni kuona jinsi gani vijana wameiva kwenye mafunzo hayo ya awali ya kijeshi lakini mafunzo hayo yanamjenga kijana kuwa tayari kujifunza mafunzo mengine ya stadi za kazi na maisha ambapo vijana watakuwa wakakamavu ,nidhamu,uhodari ,uzalendo,uvimilivu, kujiamini na moyo wa kufanya kazi hivyo kuwa tayari kulitumikia Taifa letu”Alisema
Alimshukuru na Kumpongeza Kamanda wa kikosi kwa kazi kubwa na nzuri kwa kutoa mafunzo kwa vijana ambao wametoka kwenye maeneo mbalimbali lakini weledi wa wakufunzi umefanya vijana kuwa wamoja.
“Niwapongeze vijana kwa kukubali kujiunga na Jeshi la JKT maamuzi yenu ni ya busara sana na niwatake kuheshimu na kuzingatia maamuzi yenu na kufuata yale yote mliofundishwa kwa kufanya hivyo mtakuwa mmejitendea haki wenyewe Jeshi la JKT ,jamii mlipotoka na Taifa kwa ujumla”Alisema
Awali akizungumza Mwakilishi wa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Tanzania Kanali George Barongo alisema alisema kwamba maonyesho mbalimbali ya yaluyofanywa vikundi ikiwemo ya Gwaride,singe na sanaa na yameonyesha vijana wamepata mafunzo yenye viwango vilivyokubalika vya JKT na wana kikosi wametekeleza kikamilifu majukumu makuu matatu ya JKT ambayo ni malezi ya vijana ,uzalishaji mali na ulinzi wa Taifa.
Alisema mafunzo mafunzo hayo yalianza Desemba 30, 2024 mwaka jana ambapo vijana wamejifunza mbinu mbalimbali ikiwemo mbinu za kivita,ujanja wa porini ,usomaji wa ramani,usalama na utambuzi,kupambana na majanga,silaha ndogo ndogo ,kazi za mikono na uzalishaji mali.
Alisema lengo likiwa kukuza moyo wa kizalendo na kuwajengea ukakamvu,ujasiri na uwezo wa kutumia muda vizuri na kuwafanya watambue kwamba awao ni sehemu ya jamii wanaopaswa kupata mafunzo ya JKT.
“Tumieni elimu mlioipata kutatua changamoto mbalimbali bila kuvunja sheria za nchi na niwaambie kwamba Serikali inatambua na kuthamaini umuhimu wa mafunzo ya JKt ndio maana imeendelea kuliongeza uwezo wa vijana wengi wapate kujiunga na mafunzo ya JKT”Alisema
Hata hivyo aliwataka kuhaakikisha wanazingatia nidhamu na kuifanya ikawe ndio silaha pekee dhidi ya jambo lolote litalakokuwa mbele yao.
Naye kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Mkinga Gilbert Kalima akizungumza wakati akifunga mafunzo hayo aliwataka wazazi na walezi kuacha tabia ya kuwaacha watoto kuendelea kubaki mitaani wanapomaliza shule bila kazi yoyote badala yake wawapeleke kujiunga na vyuo vya ufundi Stadi (VETA) ili waweze kupata ujuzi katika fani mbalimbali ili kuweza kujikwamua kimaisha.
Alisema kwani kuendelea kuwaacha wahitimu wa shule nyumbani bila kazi ni kutengeneza bomu ambalo baadae linaweza kuhatarisha usalama katika maeneo yao hivyo alitoa wito kwa wazazi kutumia uwepo wa chuo hicho kuwapeleka watoto wao kupata ujuzi.
Hata hivyo Kaimu Mkuu wa kikosi cha Jeshi 838 KJ, Maramba JKT Luteni Kanali Evagreen Baltazar alisema kwamba mafunzo hayo yalifunguliwa Desemba 30 mwaka jana na wameendeshwa kwa muda wa majuma 16 mfululizo.
Alisema mafunzo hayo ni kuwajengea ukakamavu ,ustahimiliv,nidhamu nzuri, uzalendo,uaminifu kupenda kazi za mikono na kumuandaa kijana kuwa sehemu ya jeshi la akiba huku akieleza vijana ha wamepata mafunzo ya ujasiriamali,ufundi na stadi za kazi katika Nyanja mbalimbaliza kilimo na ufugaji.