Na Janeth Raphael MichuziTv -Dodoma
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Ushirika Godfrey Joel Ng’urah,amemuhakikishia Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT),Emmanuel Tutuba kuwa benki hiyo itahakikisha inainua uchumi Jumuishi kwa jamii,ili kuhakikisha kila mmoja anashiriki fursa zinazotolewa na benki hiyo.
Ng’urah amesema hayo alipomtembelea ofisini kwake Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania BOT,na kufanya mazungunzo mafupi ya namna ya benki hiyo itakavyoshiriki kukuza uchumi jumuishi hapa nchini.
Amesema benki ya Ushirika imejipanga ikiwemo kuweka mikakati ya kuhakikisha kila mtanzania hususani wakulima.na wafanyabiashara wananufaika na fursa zinazotokewa na benki hapa nchini.
“Benki ya Ushirika tumejipanga kuja na sera tofauti,wananchi watarajie mambo makubwa kutoka kwenye benki hiyo,” Ng’urah.
Alisema lengo lao ni kuona jamii inanufaika na uwepo wa Benki ya Ushirika ambayo itawainua wakulima,wafanyabiashara na jamii Kwa ujumla kutokana na mikopo ambayo itakuwa inayotolewa.
Hata hivyo Mkurugenzi Mtendaji huyo,alitumia fursa hiyo kumualika rasmi Gavana kwenye Uzinduzi wa Benki ya Ushirika uliopagwa kufanyika Aprili 28 jijini hapa,ambapo mgeni rasmi anatarajia kuwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.
Hivi karibuni Waziri wa Kilimo Hussein Bashe aliwasisitiza wakulima na wafanyabiashara kuhakikisha wanafungua akauntu kwenye benki hiyi kutokana na kwamba itawasaidia kupiga hatua katika biashara mbalimbali wanazofanya zikiwemo za mazao.
Bashe amesema wakulima kupitia vyama vyao vya ushirika wanapaswa kuchangamkia kufungua akaunti katika benki ili waweze kunufaika na mikopo itakayotolewa na benki hiyo.
“Uzinduzi rasmi utafanywa na Rais DK Samia Suluhu Hassan Aprili 28,ili kuanza kazi rasmi,”amesema Bashe.
Benki hiyo inazinduliwa ikiwa na matawi manne na mawakala zaidi ya 52 kupitia vyama vya Ushirika. Pia Ni Benk ya kwanza yenye makao makuu yake Mji mkuu Dodoma