Katika jua kali la Arusha, vumbi likiwa limetanda hewani na magurudumu yakizunguka kwa kasi ya matumaini, kundi la vijana wa Kitanzania linaendelea na safari ya kipekee—Twende Butiama.
Kwa kutumia baiskeli zao, vijana kutoka mikoa mbalimbali wanapita vijiji na miji, wakibeba ujumbe mmoja muhimu: uzalendo wa kweli bado upo, na unaishi ndani ya kizazi kipya.
Lakini Twende Butiama si tu kumbukumbu ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere. Ni mwamko Ni sauti ya mshikamano, afya ya jamii, na maendeleo ya vijana kupitia michezo na usafiri John Mbise, mshiriki kutoka Arusha.
Katika kila mtaa wanaopita, vijana hawa wanakutana na wenzao wanabadilishana mawazo, wanahamasishana,juu ya yote, wanakumbusha umuhimu wa kuenzi historia na misingi ya taifa.
Kampeni hii imepata sapoti kubwa kutoka sekta binafsi, huku Vodacom Tanzania ikiongoza kama mdhamini mkuu. Kupitia vifaa, huduma za mawasiliano na motisha kwa washiriki, Vodacom imeonyesha kuwa uzalendo unaweza kuungwa mkono kwa vitendo.
Mashirika ya kijamii na serikali za mitaa pia yamepongeza harakati hizi, wakizitaja kama mfano bora wa vijana kujenga taifa kwa kushiriki moja kwa moja katika mabadiliko.
Kadri safari inavyoendelea, na kila kilomita inapopungua, ujumbe wa Twende Butiama unazidi kugusa mioyo ya Watanzania.
Tunaweza kushikamana,Tunaweza kuenzi historia yetu na tunaweza kulijenga taifa kwa misingi ya uzalendo, mshikamano na upendo wa kweli.