Na Diana Byera,Missenyi
Wananchi wa wilaya ya Missenyi,mkoani Kagera wametakiwa kuachana na dhana potofu ya kuwa ukiandika Wosia ni kujitabiria kifo badala yake waandike Wosia wakiwa hai ili kupunguza changamotoo za ugomvi wa kifamilia zinazoongezeka Kila siku .
Timu ya wataalamu wa kisheria wanaotekeleza kampeni ya msaada wa kisheria ya Mama Samia Wilayani Missenyi wametoa Elimu ya kina kwa mamia ya wananchi wa wilaya ya Missenyi waliojitokeza kuleta changamotoo zao za kisheria na kupata Elimu ya kisheria juu ya maswala mbalimbali .
Wakili wa kujitegemea na mjumbe wa Timu hiyo Jofrey Binamungu ameongoza somo la Kuandika Wosia kwa wananchi wa vijiji vya Minziro,Karagara na kigaze kata ya Minziro wilaya ya Missenyi ambapo amesema kuwa wananchi wengi na utamaduni wa wakazi wa mkoa wa Kagera wanaamini kuwa Kuandika Wosia ni kujitabiria kifo jambo ambalo Sio la kweli.
Alisema kuwa moja ya changamoto kubwa ya kisheria wanayokutana nayo kwa sasa ni maswala ya migogoro mikubwa ya kutoandika Wosia., hakuna anayejua urithi nini badala yake watu wanagombania Mali mara tu baada ya marehemu kufariki na kupelekea familia nyingi kutumia muda mwingi mahakamani na kushambuliana jambo ambalo linathorotesha uchumi wa familia nyingi za wilaya ya Missenyi.
“Utamaduni wa wakazi wa mkoa wa Kagera wanadhan ikiwa utaandika Wosia mapema utajitabiria kifo hii sio kweli ,tuandike Wosia ,tuziwasilishe katika maswala ya kisheria ili kuondoa mitafaruku ,wosia ndio nyaraka Bora kisheria ambayo haiachi Changamoto yeyote kwenye Familia ,kikubwa iwe na mashaidi ,hii itawalinda wanaoishi na wasio ishi tuepuke Dhana potofu katika hili “alisema Binamungu
Mratibu wa kampeni ya msaada wa Kisheria ya Mama Samia Maxmillan Fransis Wilayani Missenyi alipata wasaa wa kutoa elimu juu ya maswala ya Mirathi na kudai kuwa Kwa siku ya pili mfululizo toka waziri wa Katiba na Sheria Dr Damas Ndumbaro changamotoo inayoongoza kutolewa malalamiko ni mirathi .
Alisema kuwa mara nyingi watu wanaoteuliwa kusimamia Mirathi wanajimilikisha Mali na hawafiki mahakamani bali wanatumia mwanya huo kupora Ardhi na Mali za walengwa jambo ambalo limesababisha changamotoo kubwa ya ndugu na watoto kugombana.
Alitoa wito kwa wananchi wote ambao wameteuliwa kusimamia Mirathi kuhakikisha wanatambuliwa kisheria na chombo Cha mahakama na kuacha kujichukulia maamuzi ya kugawa Mali ovyoovyo kwa upendeleo jambo ambalo litaepusha migogoro Mingi ya Mirathi na kupunguza changamotoo za kushitakiana mara kwa mara.
“Imekuwa kawaida watu wanaoteuliwa kusimamia Mirathi ndio wamegeuka misiba kwa familia ,ambapo msimamizi wa Mirathi amekuwa kama Mungu mtu yeye kazi yake ni kugawa na kusimamisha utasikia leo wewe Lima wewe acha ,wakati huo atambuliwi na mahakama Wala chombo Cha kisheria na ikitokea akafariki ghafula hata familia yake inachukia ikiamini kuwa ni Mali yake ,tupunguze adha hizo na tuteue wasimamizi wa Mirathi ambao hawana tamaa”
Timu ya wataalamu wa kisheria kupitia Kampeini ya Msaada wa Kisheria wa Mama Samia wanaozunguka vijiji vya Tanzania kutoa Elimu ya kisheria na kutatua changamotoo za kisheria wanato Elimu ya kisheria kwa wananchi kwa nyanja zote zenye changamotoo,kupokea kero, kutatua changamotoo zote za kisheria na kutoa msaada wa kisheria na Leo katika wilaya ya Missenyi Kata ya Minziro mamia ya wananchi wamefurika katika viwanja vya Minziro sekondari kwa ajili ya Kupata Elimu ya maswala ya kisheria na kutatuliwa Changamotoo.