Shirika la Muungano wa Mapinduzi ya Kijani Afrika (AGRA) limeendelea kuwa mshirika mkubwa wa serikali katika mpango wa Building Better Tomorrow (BBT) unaolenga kuwainua vijana kupitia sekta ya kilimo nchini Tanzania.
Kupitia programu yake maalumu ya YEFFA (Youth Entrepreneurship For the Future of Food and Agriculture), AGRA imefanya uwekezaji mkubwa Zaidi ya mikoa 18 nchini.
Programu ya YEFFA inalenga kuwawezesha vijana, hasa wanawake, kujenga uwezo wa kijasiriamali katika kilimo cha kisasa, na kuhakikisha ushiriki wao kamili katika minyororo ya thamani ya chakula na kilimo.
Kwa kipindi cha miaka mitano AGRA imewekeza (uwekezaji ambao tayari umeanza) zaidi ya Mil 40 USD, ambazo ni zaidi ya Bil. 104 fedha za kitanzania katika kilimo nchini zaidi ikiwalenga vijana wa kike.
AGRA imekuwa ikiunga mkono mpango wa Building Better Tomorrow (BBT) kupitia ujenzi wa uwezo kwa vijana, utoaji wa mafunzo na teknolojia za kisasa za kilimo, urahisishaji wa upatikanaji wa mitaji na huduma za kifedha, pamoja na kusaidia upatikanaji wa zana na mitambo ya kisasa ya kilimo ili kuongeza ufanisi na uzalishaji.
AGRA kwa kushirikiana na serikali na wadau mbalimbali, imewafikia vijana zaidi ya 145,000 kuingia kwenye mnyororo wa thamani, masoko endelevu na jumuishi ya kilimo cha mahindi, maharage, alizeti, mpunga, na mbogamboga na kuwawezesha kufikia masoko ya nje katika nchi za DRC, Burundi na Rwanda.
Afisa wa Programu wa AGRA – Tanzania, Donald Mizambwa, amesema hayo mbele ya Waziri wa Kilimo, Mheshimiwa Hussein Bashe, wakati wa mkutano wa Wadau wanaotekeleza miradi ya kuwezesha vijana na wanawake katika sekta ya kilimo.
Mkutano huo umefanyika jijini Dodoma, ambapo Waziri Bashe alikuwa mgeni rasmi.
Waziri Bashe ameipongeza AGRA na taasisi zote zinazounga mkono juhudi za kilimo nchini, na kuzielekeza kufika katika mikoa yote ambayo haijafika ili kuhakikisha hakuna anaeachwa na fursa hii.
Mkutano wa wadau wanaotekeleza miradi ya kuwezesha vijana na wanawake katika sekta ya Kilimo-Mazao unalenga kuunganisha nguvu ya pamoja ya wadau wa maendeleo ili kutengeneza ajira nyingi,