Na Mwandishi Wetu,Dodomaa
MBUNGE wa Jimbo la Vunjo Dkt Charles Kimei ametajwa kuwa kinara wa kuzungumzia mahitaji ya wananchi kwa kuwa miongoni mwa wabunge vinara wa kusema, kuchangia au kuhoji katika kila kikao cha bunge la 12 linalotarajiwa kuvunjwa mwishoni mwa mwezi Juni mwaka huu.
Kwa mujibu wa tovuti ya Bunge la Tanzania inaonyesha Dk.Kimei amechangia mara 49 na kuuliza maswali 110 yanayohusu jimboni na yanayogusa Taifa kwa ujumla.
Mbunge huyo ni aina ya viongozi wanaoipenda kazi yao na kuguswa ambao wamekuwa wakioonekana katika majimbo yao wakifanya mikutano ya wananchi kutoa mrejesho, kusikiliza na kutatua kero pamoja na ziara za ukaguzi wa miradi ya maendeleo.
Miongoni mwa maswali ambayo Dkt.Kimei ameweza kuuliza Bungeni ni pamoja na aliloulizwa kupitia Wizara ya Viwanda ambapo alihoji kuhusu Shirika la Viwanda Vidogo (SIDO) ambapo alieleza kuwa taasisi hiyo inalenga watu wa chini watu ambao wapo kwenye vijiji na kadhalika na hawa watu ni vigumu sana waweze kuelewa hivi vitu alivyovieleza kwa sababu hata mimi nilikuwa sivijui. Je, wana mpango gani wa kuiongezea SIDO uwezo wa kujitangaza na kutekeleza maonesho kwenye miji midogo midogo kama Mji wa Himo? .
Mbali na hilo pia alihoji kuhusu swali kuhusiana na mabanda ya viwanda au majengo ya viwanda
” Kasi ya ujengaji wa majengo hayo ni ndogo sana pengine tunaenda na too much sophistication, lakini tukienda kwa mtindo mwingine naamini tutaweza tukaharakisha sana ujenzi wa haya mabanda. Je, kama wakienda na kasi hii kweli ni lini wanafikiria watatufikia sisi kule kwenye Mji wa Himo, Uchira na miji midogo midogo kwenye mikoa yetu?.,”