Na Pamela Mollel,Arusha
Watumiaji wote wa Tehama wametakiwa kuhakikisha wanajilinda wao pamoja na vifaa wanavyovitumia ili kuepusha taarifaa zao kuingiliwa.
Rai hiyo ilitolewa hivi karibu jijini Arusha na Mtaalamu wa Tehama kutoka Tasaf, Peter Lwanda katika kongamano la usalama mtandaoni
“Tujitaidi kujilinda kwa kuwa sasahivi teknolojia imekuwa kwa kasi kubwa hivyo ni muhimu kulinda hata vifaa tunavyotumia ikiwemo simu zetu za mkononi,komputa na vifaa vingine”Anasema Lwanda
Amesema kupitia kongamano hilo lililowaleta watumiaji wa Tehama pamoja kutoka ndani ya nchi na nje ya nchi itasaidia katika kukabiliana na mashambulizi ya Tehama ambayo ni vita kubwa kuliko hata ya kutumia silaha,kwakuwa wanaoshambulia wanaweza kushambulia miundombinu muhimu ya Taifa
“Washambuliaji wanaweza kuingilia mfumo ikiwemo vyanzo vya umeme na Nchi ikakosa umeme lakini pia hata miradi mingine “Anasema Lwanda
Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo kutoka mfuko wa fidia kwa wafanyakazi,Stephen Goyayi anasema wataendelea kutoa elimu kwa wafanyakazi ili waweze kujilinda
Aidha ameongeza kuwa mfuko huo unafanya kazi kwa kutoa huduma kupitia mtandao hivyo wataendelea kulelimisha kuhusu maswala mbalimbali ya mtandaoni