Taasisi ya GH Foundation imefanikiwa kufanya warsha ya kuwajengea uwezo askari polisi, Maafisa ustawi wa jamii, waandishi wa habari na viongozi wa dini katika Kupambana na Ukatili wa Kijinsia. Gifted Heart Foundation inayoongozwa na Godlisten Malisa iliwajengea uwezo huo kupitia warsha iliyofanyika wiki iliyopita katika ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam ikiwa na lengo la kuboresha mifumo na kuimarisha ushirikiano baina ya wadau mbalimbali wa kupambana na Ukatili wa Kijinsia.
Warsha hiyo ilifanyika ikilenga kuongeza ufanisi katika kushughulikia vitendo vya ukatili kwa kuwajengea uwezo maafisa wa polisi, maafisa wa ustawi wa jamii, na viongozi wa dini, mashirika yasiyo ya kiserikali na vyombo vya habari katika kupambana na ukatili wa kijinsia.
Warsha hiyo ni sehemu ya jitihada za taaasisi ya GH Foundation kutekeleza afua zake mbili ambazo ni kupambana na magonjwa yasiyoambukiza na kupambana na Ukatili wa Kijinsia ili kukuza usawa na ujumuishaji katika kijamii.