Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC), Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa na Mjumbe wa Kamati Kuu, Ndg. Rabia Abdalla Hamid, Aprili 22, 2025 ameungana na viongozi wa vyama vingine vya siasa kutoka nchi mbalimbali kuweka maua na kutembelea makumbusho ya Kiongozi na Mwanamapinduzi wa Russia na lililokuwa Shirikisho la Kisovieti, Vladimir Lenin, katika jiji la Moscow.
Ndg. Rabia yupo Moscow, kushiriki Mkutano wa Kimataifa wa Jukwaa la Kupinga Ufashisti, kufuatia mwaliko wa Chama Cha Kikomunisti cha Shirikisho la Russia (CPRF). Mkutano huo ulianza Aprili 22 na utafungwa Aprili 25, 2025.