Na Diana Byera,Missenyi
Zaidi wa wanafunzi 700 wa shule ya sekondari Mtukula Wamepewa Elimu ya kuwasilisha na kurepoti matukio ya ukatili katika madawati mbalimbali wilayani Missenyi huku wakihaidiwa Ulinzi wa kutowaweka wazi pale watakapotoa taarifa.
Timu ya uratibu wa kampeni ya msaada wa kisheria ya mama Samia wilayani Missenyi imefika shuleni hapo kama sehemu ya kutoa Elimu ya kisheria juu ya maswala ya ukatili kwa watoto ambapo Wanafunzi wengi ni waathirika wakubwa wa matukio ya Ubakaji na ulawiti pamoja na mimba za utotoni
Mjumbe wa kamati ya kampeni ya msaada wa kisheria ya mama ambaye ni Afisa wa Dawati la Jinsia kitengo Cha Polisi Kyaka wilayani Missenyi Grace Matofali Ametoa wito kwa wanafunzi wanakabiliwa na matukio ya ukatili kutokukaa kimya badala yake wafike katika madawati yaliyoandaliwa Kwa ajili ya Kupata ufumbuzi
Alisema kuwa hakuna Siri itakayofika kwa mtu yeyote au kumutaja mwathirika wa tukio la ubakaji wa ulawiti pale atakapokuwa Ametoa Taarifa .
“Najua mnapokea vitisho vingi vya kahawa na watu wanaowafanyia ukatili ,anasema ukisema nitakuua ,hakuna atakaye kuua njoo unipe Taarifa serikali itakulinda kwa nguvu zote msikubari kutumika njooni mtoe taarifa mama Samia yuko kwa ajili yenu”alisema Matofali.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari Mtukula wametoa Pongezi kwa Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuboresha Miundo mbinu ya shule na kuteua shule yao kufikiwa na Elimu juu ya maswala ya kisheria yanayohusu Ukatili kwani wanafunzi wengi wanakabiriwa na vitisho kutoka kwa waharifu wenye Nia ovu ya kutenda makosa ya ukatili kwa watoto.