Na Diana Byera,Missenyi,
Wenyeviti wa vijiji vya Mtukula ,Byeju,Nkerenge kata ya Mtukula wilaya ya Missenyi wameishukuru serikali kwa Kuona Elimu ya Kisheria inafaa kuwafikia wananchi wote wa vijijini Wilayani Missenyi, kupitia wenyeviti wao kwani wenyeviti wengi wanaupungufu kuhusu maswala ya Sheria kwani changamoto nyingi zinazowakabiri Wanachi zinatokana na kutojua Sheria vizuri.
Timu ya wataalamu wanaoratibu kampeni ya msaada wa kisheria ya mama Samia wilayani Missenyi,imefanya mafunzo na utatuzi wa migogoro wa kisheria katika vijiji hivyo ambapo wenyeviti wengi wa vijiji wamekuwa wakitimiza wajibu wao wa kutoa huduma kwa wananchi lakini mara nyingi wamejikuta wakivunja Sheria bila kujua.
Oscar Evarsta mwenyekiti wa Kijiji Cha mtukula alisema Kampeini hii ni muhimu sana na serikali imefikiria mbali sana na Kuona mahitaji ya sasa ya wananchi kwani Wenyeviti ndio wanaongoza wananchi lakini asilimia kubwa ya wenyeviti wanaupungufu wa Sheria hivyo changamoto nyingi za Wanachi zinaongezeka na migogoro mingi inababishwa na kutokujua Sheria.
Alitoa wito kwa timu hiyo kuomba mafunzo ya Sheria kuwa endelevu ili kupunguza changamoto za uvunjifu wa Sheria ambazo zimekuwa zikijitokeza na kuondoa changamoto za familia nyingi kupelekana mahakamani kwani wakiwa na Elimu ya kutosha migogoro Mingi itasuruhishwa kifamilia bila kupoteza muda Mahakamani
Mwenyekiti Kijiji Cha Byeju Patrick Deogratias kata mtukula alisema kuwa wenyeviti wamekuwa kama sehemu ya mahakama ndogo hivyo wanasukuhisha migogoro ya ndoa ,Aridhi,Ugomvi,wizi na saa nyingine wanahusika kuvunja Sheria kwa kuwalinda wapiga kura wao.
Ameipongeza Elimu ya kisheria ambayo imeongeza uelewa juu ya maswala ya Aridhi,Kuandika Wosia , kupata hati miliki ambapo alidai kuwa pamoja na serikali kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo swala la Kupita vijiji vya pembezoni na kutoa Elimu pamoja na kutatua migogoro imeongeza Morali ya wananchi kuendelea kuipenda serikali yao.
Katibu wa chama Cha Mapinduzi CCM Tawi la Mtukula ameipongeza serikali ya awamu ya 6 kutoa Elimu Hiyo ya kisheria na kuomba kuwa endelevu kwani Vijiji vingi vinavyopakana na mipaka ya nchi nyingine vinakumbana na uvunjifu mkubwa wa Sheria.
Alisema uwepo wa kampeni ya msaada wa kisheria ya mama Samia imeongeza Imani kubwa katika chama hicho kwani kupitia Kampeinu hiyo ameshuhudia wananchi wasio na uwezo wanasaidika na kutatuliwa Changamoto zao hivyo kama kampeini hiyo itakuwa Endeleavu wananchi wengi watasaidika na kupunguza kwenda kupanga foleni mahakamani
Taaarifa iliyotolewa na mratibu wa kampeini ya msaada wa kisheria Wilaya ya Missenyi Maxmillan Fransis alisema kuwa tayari vijiji 30 vya wilaya ya Missenyi vimefikiwa na kampeini ya msaada wa kisheria na tayari wizara ya Katiba na Sheria imeongeza Siku 5 wilayani humo kwa ajili ya wananchi kuongezewa Elimu zaidi ya kisheria na kutatua changamotoo za kisheria Zilizojitokeza.
“Waziri wa Katiba na Sheria alifungua kampieni ya msaada wa kisheria ya mama Samia Aprili 14 Hadi 23 mkoani Kagera ikiwemo wilaya ya Missenyi lakin baada ya kuona bado Kuna uhitaji wa Elimu hiyo na wananchi wanauhitaji wa kutatuliwa Changamoto zao za kisheria hawana uwezo wa kuwalipa mawakili wameongeza siku 5 nyingine za Kuwahudumia Wanachi hivyo wilaya ya Missenyi tutafikia vijiji 45 Hadi kufikia Aprili 28″alisema Fransis.