

Wajumbe wa Bodi ya TASAC wakiangalia ujenzi wa maboresho ya Bandari ya Bukoba wakati walipofanya ziara katika Bandari hiyo.
Bodi ya Wakurugenzi wa TASAC ,Watumishi wa TASAC,TPA wakiwa katika bandari ya Kemondo.
Baadhi picha katika Matukio ya bodi ya TASAC katika Bandari ya Kemondo na Bukoba.
Na Mwandishi Wetu ,Bukoba
BODI ya Wakurugenzi wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limesema kuwa Serikali imewekeza fedha nyingi katika miradi ya ujenzo wa Bandari za Kemondo na Bukoba hivyo fedha hizo zinatakiwa kuleta tija na zirudi kutokana huduma zitazotolewa na Bandari hizo.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati ziara Bodi katika Bandari hizo Mwenyekiti wa Bodi hiyo Nah.Mussa Mandia amesema kuwa baada ya maboresho ya miundombinu ya ujenzi wa bandari watahudumia mizigo na abiria kwa kiwango kikubwa ikilinganishwa na ilivyokuwa awali.
Amessema kuwa fedha ya Bandari ya Kemondo bilioni 20 na ujenzi wake umekamilika ambapo huduma zake zimeongezeka hadi kufikia tani 150000 kwa mwezi na mapato yake yameongezeka mara tatu huku Bandari ya Bukoba ujenzi wake ukiwa katika hatua za mwisho unaogharimu zaidi ya sh.Bilioni 19.
Amesema kuwa kama wadhibiti ni kuhakikisha Bandari hizo zinaendelea kutoa huduma bora na tija kwa serikali huku akitaka wasimamizi wa bandari kusimamia kwa weledi.
Amesema Serikali ya awamu ya Sita ya Dkt.Samia Suluhu Hassan imeweza kutimiza ndoto katika upanuzi wa bandari za Kemondo na Bukoba ambayo miundombinu yake ilikuwa ya zamani ambapo haiendani na mahitaji ya sasa.
Hata hivyo amesema kazi bodi itaendelea kushauri katika taasisi wanayoidhibiti ambapo matokeo yake yanaonekana kwa miradi mbalimbali kwenye bandari nchi nzima
Mkuu wa Bandari ya Bukoba wa TPA Malick Ismail amesema kuwa Bandari hiyo maboresho ya ujenzi bandari hiyo baada ya kukamilika watahudumia meli nne kwa wakati mmoja tofauti na ilivyokuwa awali ambapo walikuwa wakihudumia meli moja.