Na Janeth Raphael MichuziTv -Dodoma
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule,,amewataka wafanya biashara kujitokeza kushiriki kongamano la kitaifa la wanaushirika,litakalolenga kujadili fursa mbalimbali za uwekezaji katika sekta ya kilimo na ushirika.
Kongamano hilo limepangwa kufanyika Aprili 29 Mwaka huu katika ukumbi wa Jakaya Kikwete uliopo mkoani humo ,huku viongozi mbalimbali wakitarajia kushiriki katika kongamano hilo.
Senyamule amesema hayo leo katika mkutano na waandiishi.wa habari uliofanyika jana jjini Dodoma huku akisisitiza ikini Dodoma wenye lengo la kuzungumzia kuhusiana na fursa zitakazotolewa na benki ya ushirika.
“Naomba wafanyabiashara na wanaushirika wajitokeze kwa wingi kushiriki katika kongamano hilo ambalo litakuwa la kihistoria kutokana na mada zirakazojadiliwa,” Senyamule.
Akizungumzia kuhusiana na uzinduzi wa benki ya Ushirika alisema itasimikwa kwenye misingi ya Ushirika, uchumi shirikishi na maendeleo ya pamoja hivyo kuifanya kuwa chombo cha kuwezesha maendeleo ya kiuchumi kwa watu wa kawaida katika jamii.
Senyamule amesema mgeni rasmi katika uzinduzi wa kongamano hilo anatarajia kuwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,uzinduzi rasmi wa benki ya ushirika utafanyika Aprili 28 chini ya Rais DK Samia Suluhu Hassan.
Amesema benki hiyo ni ya kipekee inayomilikiwa kwa ubia na Vyama vya Ushirika, wanachama wao, vikundi vya kijamii na Taasisi za Ushirika kutoka hapa nchini.
Amesema katika misingi ya ushirika, uchumi shirikishi na maendeleo ya pamoja kupitia mfumo wa umiliki wa hisa, kila Mtanzania anayo nafasi ya kuwa sehemu ya mafanikio ya benki hii ikiwa ni chombo cha kuwezesha maendeleo
Aidha, Senyamule ameongeza kuwa Benki hiyo inaanza rasmi kazi zake ikiwa na Matawi manne (4) katika Mikoa ya Dodoma, Kilimanjaro, Mtwara (Tandahimba) na Tabora, sambamba na mawakala zaidi ya 52 waliopo katika vijiji na miji mbalimbali.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Godfrey Ng’urah, amesema Benki hiyo ni ya kibiashara kwa wanaushirika hivyo, itachagiza shughuli za kilimo, shughuli za kinamama, kuongeza thamani ya mazao pamoja na shughuli za biashara kwa wafanyabiashara wadogo na wa kati pamoja na kurudisha enzi za ushirika katika nchi.
Uzinduzi huo utatanguliwa na Kongamano la Kitaifa la wanaushirika Aprili 27, 2025 likiwa na mada kuu: