Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe. Mohamed Mchengerwa leo Aprili 26, 2025 amewasili Mkoani Mbeya kwa ajili ya kuanza ziara ya kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.
Aidha, leo kiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Muungano hapa nchini tayari amepata fursa ya kukagua miradi mikubwa ya kisasa ya ujenzi wa soko kubwa la soko Matola na stendi ya kisasa ya mabasi.
Katika ziara hiyo Mkuu wa Mkoa wa Mbeya ameongozana na Mhe. Waziri Mchengerwa ambapo amemshukuru Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi katika miradi ya maendeleo.
Aidha, Mhe. Mchengerwa amewapongeza wakandarasi wazawa kwa kufanya kazi kwa ufanisi katika miradi hiyo huku akiwataka kuendelea kufanya kazi kwa kutanguliza uzalendo.