Afisa Miradi wa EfG, Bi. Susan Sitta
Na Kadama Malunde – Malunde 1 Blog
Shirika lisilo la kiserikali la Equality for Growth (EfG) limeendesha mafunzo kuhusu Usawa wa Kijinsia, Uongozi na Haki za Kiraia kwa wanawake wafanyabiashara wa masoko mbalimbali katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.
Mafunzo hayo ya siku mbili (Mei 1-2, 2025) yanafanyika katika ukumbi wa Liga Hotel mjini Shinyanga, yakiwaleta pamoja wanawake wafanyabiashara kutoka masoko sita ya Manispaa ya Shinyanga ( Soko Kuu, Ibinzamata, Ngokolo, Kambarage, Nguzo Nane na Majengo Mapya).
Akizungumza wakati wa mafunzo hayo yaliyofadhiliwa na Ford Foundation, Afisa Miradi wa EfG, Bi. Susan Sitta, amesema lengo kuu ni kuwajengea uwezo wanawake wafanyabiashara kushiriki kikamilifu katika nafasi za uongozi, kufanya maamuzi na kusimamia shughuli za kibiashara katika mazingira ya soko.
“Tunataka kuona wanawake wakiongoza, wakielewa haki zao na wakihusika moja kwa moja katika kupanga na kusimamia ajenda zinazowagusa. Mafunzo haya ni sehemu ya mchakato wa kuwawezesha,” amesema Bi. Suzan.
Ameongeza kuwa mafunzo hayo ni sehemu ya utekelezaji wa Programu ya Sauti ya Mwanamke Sokoni, iliyoanzishwa Oktoba 2011, na ambayo hadi sasa imetekelezwa katika zaidi ya masoko 47 katika mikoa 10 nchini Tanzania, ikiwemo Dar es Salaam, Mwanza, Shinyanga, Lindi, Mtwara, Mbeya, Iringa, Tanga (Lushoto), Musoma na Dodoma.
Kwa upande wake, Afisa Utawala wa EfG, Bi. Evah Buhembo, amewatia moyo wanawake hao kuendeleza ushirikiano wao kwa kujiunga kwenye vikundi ili waweze kunufaika na fursa za mikopo kutoka halmashauri, na hivyo kuimarisha biashara zao na kujenga uongozi thabiti ndani ya jamii ya wafanyabiashara.
“Kupitia ushirikiano na vikundi, wanawake wanaweza kupata mikopo, kushirikishana maarifa na kusimama imara kama viongozi katika maeneo yao ya biashara,” amesema Bi. Evah.
EfG ni shirika lisilo la kiserikali lililosajiliwa rasmi tarehe 6 Agosti 2008, likiwa na dhamira ya kuinua sekta isiyo rasmi, hasa kwa wanawake, kwa kutoa mafunzo ya sheria na haki za binadamu, msaada wa kisheria, kuwezesha usawa wa kijinsia katika fursa za kibiashara, na kushawishi sera zinazolenga maendeleo jumuishi.
Afisa Miradi wa EfG, Bi. Susan Sitta akizungumza wakati wa
mafunzo kuhusu Usawa wa Kijinsia, Uongozi na Haki za Kiraia kwa wanawake wafanyabiashara wa masoko mbalimbali katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.

Afisa Utawala wa EfG, Bi. Evah Buhembo akitoa mada kuhusu Uongozi na Haki za Kiraia wakati wa mafunzo kuhusu Usawa wa Kijinsia, Uongozi na Haki za Kiraia kwa wanawake wafanyabiashara wa masoko mbalimbali katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.

Afisa Program wa EfG, Nandipa Shadrack akitoa mada kuhusu Usawa wa Kijinsia wakati wa mafunzo kuhusu Usawa wa Kijinsia, Uongozi na Haki za Kiraia kwa wanawake wafanyabiashara wa masoko mbalimbali katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.

Mshiriki wa mafunzo akichangia hoja wakati Afisa Program wa EfG, Nandipa Shadrack akitoa mada kuhusu Usawa wa Kijinsia kwenye mafunzo kuhusu Usawa wa Kijinsia, Uongozi na Haki za Kiraia kwa wanawake wafanyabiashara wa masoko mbalimbali katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.
Wanawake wafanyabiashara sokoni wakifuatilia mafunzo kuhusu Usawa wa Kijinsia, Uongozi na Haki za Kiraia