Farida Mangube, Morogoro
Katibu wa Itikadi na uenezi Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa CPA Amos Makala anatarajia kufanya ziara ya siku Sita mkoani Morogoro ambapo atakuana na kuzungumza na wanachama wa CCM pamoja na wananchi na kuelezea utekelezaji wa ilani ya CCM.
Taarifa ya ziara ya kiongozi huyo imetolewa na Msemaji wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Morogoro Zangina Zangina wakati akizungumza na Waandishi wa Habari Ofisini kwake.
Amesema CPA Makala anatazamiwa kuanza ziara hiyo Mei 05 hadi 11, ambapo ataanza ziara yake Wilaya ya Morogoro kwa Halmashauri zake zote mbili, baadae ataelekea Wilaya ya Mvomero, Ulanga, Kilosa, Kilombero, Malinyi na kuhitimisha wilayani Gairo.