Dar es Salaam, Mei 6, 2025 – Kama sehemu ya maadhimisho ya miaka 30 ya tokea kuanzishwa kwake, Benki ya CRDB imeandaa Kongamano la Wawekezaji jijini Dar es Salaam katika hoteli ya Johari Rotana, lililohudhuriwa na wawekezaji 200 wa taasisi na binafsi kuangazia utendaji wa benki hiyo, kupitia matokeo ya kifedha yaliyokaguliwa ya 2024, na kujadili matokeo ya utekelezaji wa mkakati wake wa biashara, ikiwamo matokeo ya fedha ya robo ya Kwanza ya 2025.
Kongamano hilo lilihudhuriwa na Balozi wa Denmark nchini, Mheshimiwa Jasper Kammersgaard, Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya CRDB, Dkt. Ally Hussein Laay, na kuongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kundi la Benki ya CRDB, Abdulmajid Mussa Nsekela, ambaye aliwasilisha mada juu ya utendaji wa benki hiyo, pamoja utekelezaji wa mikakati yake, na malengo ya baadaye.
Faida Kubwa Zaidi Katika Miaka 30
Katika hotuba yake, Nsekela aliwajulisha wawekezaji kuwa Kundi la Benki ya CRDB lilipata faida baada ya kodi kubwa zaidi katika historia yake ya Shilingi bilioni 551 mwaka 2024, ikiwa ni ongezeko la asilimia 30.3 ikilinganishwa na mwaka uliopita 2023.
“Matokeo haya ya kihistoria ni ushahidi wa miaka 30 ya uongozi, ubunifu, na ubora wa huduma za kibenki,” alisema Nsekela. “Yanaonyesha si tu nguvu ya hali yetu ya kifedha bali pia maisha tuliyogusa, biashara tulizowezesha, na uchumi tunaounga mkono katika kanda nzima.”
Jumla ya mali iliongezeka kwa asilimia 24.5 kufikia Shilingi bilioni 16.7 trilioni, ikichochewa na ukuaji wa mikopo na ukusanyaji wa amana. Mikopo iliongezeka kwa asilimia 22.8 kufikia Shilingi 10.4 trilioni, ikisababishwa na usimamizi mzuri wa vihatarishi vya mikopo na mahitaji makubwa kutoka kwa sekta za biashara, wajasiriamali, na kilimo. Amana za wateja zilikua na kufikia Shilingi 10.9 trilioni, na asilimia 87 ikiwa ni amana za gharama nafuu (CASA). Kampuni tanzu za Benki ya CRDB zilichangia asilimia 6 katika faida baada ya kodi ya kundi:
· Benki ya CRDB Burundi ilipata faida baada ya kodi ya Shilingi bilioni 40.3, ikiwa na jumla ya mali Shilingi trilioni 1.5.
· CRDB Insurance, ikiwa ni mwaka wake wa kwanza, iliripoti faida ya Shilingi milioni 343, i kuongeza mapato ya kundi ya kando ya riba.
· Benki ya CRDB Congo, ingawa iko katika hatua za mwanzo, ilionyesha maendeleo mazuri, ikiwa na jumla ya mali za Shilingi bilioni ilipata hasara ya Shilingi bilioni 6.5 chini ya kiwango kilichotarajiwa. Matarajio ni kuona benki hii ikipata faida mapema zaidi ya makadirio ya awali.
· Kupitia Taasisi ya CRDB Foundation, Benki ya CRDB iliendelea na juhudi za ujumuishi wa kifedha, hususani wanawake na vijana zaidi ya milioni 1 kupitia mpango wa IMBEJU, ukiimarisha ahadi ya Benki katika kuchochea ujumuishi wa kifedha.
Uwekezaji katika Mifumo ya Kidijitali na Ukuaji wa Wateja

Uwekezaji katika mifumo ya kidijitali umeendelea kuwa nguzo ya mikakati ya Benki ya CRDB, ambapo asilimia 98 ya miamala yote ya wateja mwaka 2024 ilifanyika kupitia njia mbadala. Kati ya hizi, asilimia 53 zilifanyika kupitia majukwaa ya kidijitali ikiwa ni pamoja na SimBanking, ambapo ilitoa mikopo ya kidijitali zaidi ya Shilingi bilioni 18, wakati asilimia 45 ya miamala ilifanyika kupitia CRDB Wakala. Ni asilimia 2 tu ya miamala ilifanyika kupitia matawi, ikionyesha mafanikio ya miakati ya Kundi la Benki ya CRDB.
Benki ilishuhudia ongezeko la wateja wapya milioni 1.5 kwa mwaka 2024, ikiwa ni pamoja na zaidi ya 340,000 kupitia CRDB Al Barakah, dirisha la benki ya Kiislamu. Tafiti zilizofanywa na wakaguzi huru zinaonyesha kuridhika wa wateja kwa asilimia 94, ikiwa ni ishara ya utoaji wa huduma bora na urahisi wa kidijitali.

Ubora wa Uendeshaji
Nsekela anabainisha kuwa Kundi la Benki ya CRDB lilishuhudia Uwiano wa Mikopo Chechefu wa asilimia 2.9, ikiwa ndani ya viwango vya udhibiti, faida ya mtaji ilikuwa asilimia 28. Uwiano wa gharama kwa mapato uliboreshwa hadi 45.9%, ikionyesha ufanisi wa kiutendaji. Uwezo wa mtaji ulikuwa asilimia 17.2, ukihakikisha ustahimilivu kwa upanuzi wa baadaye.
Matokeo ya Ushirikiano wa Kimkakati
Benki ya CRDB liliendelea kufungua fursa za kiuchumi kupitia ushirikiano wa kimkakati, ikikusanya zaidi ya Dola za Marekani Milioni 700 kusaidia sekta muhimu, ikiwa ni pamoja na Dola za Marekani Milioni 45 zilizoelekezwa kusaidia biashara za kikanda katika sekta muhimu kupitia kampuni tanzu za Burundi na DR Congo. Juhudi hizi zilichangia kuzalishwa kwa ajira zaidi ya 10,000.
“Matokeo ya haya ya ujumuishi wa kifedha na kiuchimu ni ishara ya mikakati thabiti ya ushirikano wa washirika wetu wa ndani na wa kimataifa,” alisema Nsekela. “Iwe ni kupitia fedha za biashara, uwezeshaji wa vijana, au uwekezaji wa kijani, tumejikita katika kujenga ustawi kwa wote.”

Gawio na Matokeo ya Robo ya Kwanza 2025
Akielezea kuhusu mafanikio ya Kundi, Nsekela alisema Bodi ya Wakiurugenzi ya benki hiyo imependekeza ongezeko la asilimia 30 katika gawio kwa kila hisa, kutoka Shilingi 50 hadi Shilingi 65 kwa hisa, ikiendelea kutengeneza thamani endelevu kwa wanahisa kutokana na uwekezaji wao.
Kongamano hilo pia lilijadili matokeo ya kifedha ya Robo ya Kwanza ya 2025, ambayo yalionyesha ukuaji endelevu, ambapo Benki ya CRDB na kampuni zake tanzu zilipata faida baada ya kodi ya Shilingi bilioni 173, ikiwa ni ongezeko la asilimia 36 ikilinganishwa na Robo ya Kwanza ya 2024. Mapato ya riba yaliongezeka hadi Shilingi bilioni 308, ikionyesha mweleko mzuri wa kiutendaji wa Kundi.
“Tuna furaha kutangaza mwanzo mzuri wa 2025,” alisema Nsekela. “Tunaendelea na lengo letu la kuharakisha mabadiliko ya kidijitali, kupanua uwekezaji wetu wa kikanda, na kuimarisha uwezeshaji wetu kwa wajasiriamali hususan wetu vijana na wanawake, pamoja na kuboresha mikakati yetu katika kufadhili miradi ya kijani na ile inayozingatia mabadiliko ya tabia nchi.”

Akizungumza katika kongamano hilo Mwenyekiti wa Bodi, Dkt. Ally Laay, amewaahidi wawekezaji kuwa Bodi ya Wakurugenzi itaendelea kuweka sera na miongozo itakayochchea ukuaji endelevu na muda mrefu. “Tunaposherehekea miaka 30 ya safari ya Benki ya CRDB, matokeo haya yanathibitisha uwazi wa kimkakati na ustahimilivu wetu. Tuna msingi imara unaowezesha ukuaji wa baadaye, hivyo niwaombe wawekezaji kuendelea kuwekeza na kuiamini benki yao,” alisema Dkt. Laay.
Dkt. Laay pia alitumia fursa hiyo kuwaalika wanahisa wa Benki ya CRDB katika Mkutano Mkuu wa 30, utakaofanyika tarehe 17 Mei 2025, katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC). Mkutano Mkuu huo utatanguliwa na Semina ya Wanahisa, ambapo Mgeni rasmi atakuwa Makamu wa Rais, Dkt. Philip Isidor Mpango. “Hii ni fursa adhimu kwetu kusherehekea kwa pamoja mafanikio tuliyoyapata katika safari yetu ya miaka 30. Ni matumaini yangu kuwa tutajitokeza kwa wingi,” alimaliza Dkt. Laay.
Katika kongamano hilo, wawekezaji walionekana kuvutiwa na utendaji wa Benki hiyo na uwazi katika mikakati yake ya biashara ya baadae. “Benki ya CRDB inaendelea kuvutia kwa uendelevu wake wa utendaji mzuri, uwazi wa malengo, na mkakati thabiti ya kikanda,” alisema Prof. Mohammed Warsame, Mkurugenzi Mtendaji wa iTrust. “Inatia moyo kuona benki ya Kitanzania ikijiimarisha kikanda kwa kupitia ubunifu na mikakati madhubuti.”