MVOMERO: Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), CPA Amos Makalla amepiga goti kuwaomba wananchi wa Mvomero kumruhusu kutogombea tena jimbo hilo na kuwaomba wamruhusu aendelee na jukumu alilonalo la Uenezi.
Makalla ameeleza hayo leo Mei 7,2025 wakati akizungumza na wananchi katika eneo la Turiani Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro, ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya siku saba katika mkoa huo.
Awali Makalla amewashukuru wananchi wa Mvomero kwa heshima waliyompa 2010 ya kuwa Mbunge na 2020 walimpa heshima kubwa ya kuongoza katika kura za maoni na yote hiyo ni kwa sababu walifanya kazi vizuri aliyoipokea kutoka kwa mtangulizi wake Murad Sadiq.
Aidha, Makalla amesema pamoja na heshima wananchi hao waliyompatia nyakati zote aliwaomba wamruhusu aendelee kumsaidi Mwenyekiti wa CCM ambaye ni Rais Samia Suluhu Hassan katika nafasi aliyompa ya uenezi hususani kuelekea katika uchaguzi mkuu.
Amesema mwenyekiti wa chama amempe heshima kubwa na anahitaji kuifanyia kazi kwa asilimia 100, hivyo alieleza kutokushiriki katika kugombea nafasi ya ubunge kwenye jimbo hilo na kuwaombe waipokee uamuzi huo.
Pia ameahidi akiwa katika nafasi hiyo ya Uenezi ataendelea kusimamia barabara ya kutoka Mvomera kwenda Handeni kuhakikisha inaekelezwa
Makalla ameeleza hayo akijibu hoja iliyoelezwa na Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Jonas Van Zeeland alisema kutokana na Makalla kumpa heshima na ushirikiano pale mwaka 2020 pamoja na kuongoza kwake katika kura za maoni na kutokana na nafasi aliyompa yupo tayari kumuacha Makalla agombee ubunge katika jimbo hilo.