Taasisi ya Elimu Tanzania imeshiriki katika mkutano wa kimataifa wa 18 na maonesho ya Elimu ya kidigitali ambapo Washiriki kutoka nchi 65 wanashiriki (E- Learning Africa) katika kituo cha kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es laam,Leo tarehe 7.5.2025.
Mkutano huo umeambatana na maonesho ambapo Taasisi mbalimbali za ndani na nje ya nchi zinashiriki kuonesha teknolojia zake katika kusaidia ukuaji wa Sekta ya Elimu.
Mkurugenzi Mkuu wa TET, Dkt. Aneth Komba ameshiriki katika mkutano huo na kutembelea katika banda la maonesho la Taasisi ya Elimu Tanzania kujionea shughuli mbalimbali zinazoendelea katika kuwahudumia washiriki mbalimbali.
Katika Mkutano huo, TET imepata nafasi ya kuonesha teknolojia zake ikiwemo teknolojia ya SMART CLASS, LMS (Learning Management system) pamoja na Digital Library namna zinavyosaidia katika ujifunzaji na ufundishaji nchini.