RUAHA: Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo (CCM),CPA Amos Makallla amewaomba wananchi wa jimbo la Mikumi kukiunga mkono chama hicho, katika uchaguzi mkuu .
CPA Makalla ametoa kauli hiyo leo Alhamisi wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Ruaha Jimbo la Mikumi wilayani Kilosa aliposimama kuwasalimia akielekea Kilombero.
Makalla amesema hapo zamani wananchi wa Morogoro katika majimbo ya Kilombero, Mikumi na Mlimba walionjeshwa sumu, lakini hivi sasa waliowaonjesha( Chadema) hawatashiriki tena.
Kutokana na hilo, CPA Makalla amewataka wananchi wa Morogoro kwa kujiandikisha ili kupata fursa ya kushiriki katika uchaguzi mkuu ili kukiwezesha cham hicho kupTa ushindi mnono.
Chama cha Mapinduzi (CCM) kimesema kitendo cha Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kutoshiriki uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu ni mserereko wa ushindi kwa chama hicho tawala.