
Rais Dkt. Mwinyi amefika nyumbani kwa marehemu, Mtaa wa Kibamba CCM, Wilaya ya Ubungo, jijini Dar es Salaam, kutoa mkono wa pole kwa mjane wa marehemu, Bi Sarah Mwakanjuki, pamoja na wanafamilia, ndugu, jamaa na marafiki.
Rais Dkt. Mwinyi amewataka wote walioguswa na msiba huo kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.
Marehemu Charles Hillary amefariki akiwa na umri wa miaka 66.
Rais Dkt. Mwinyi alimteua kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano Ikulu tarehe 30 Desemba 2021, na baadaye akamteua tena kuwa Msemaji Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar tarehe 6 Februari 2023.