Na.Mwandishi Wetu – Arusha
Benki ya CRDB imepata faida ya Gawio la shilingi bilioni 551 baada ya Kodi kwa mwaka 2025 tofauti na shilingi bilioni 450 ambazo benki hiyo ilipata faida mwaka 2024.
Aidha benki hiyo inatarajia kutumia kiasi Cha shilingi bilioni 169.8 ikiwa zitaidhinishwa na mkutano mkuu wa wanahisa kwa ajili ya Gawio la shilingi 65 kila hisa sawa na ongezeko la asilimia 30 ambapo ni mapendekezo ya bodi ya CRDB.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Arusha Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Dkt.Ally Laay wakati wa kuelekea mkutano mkuu wa mwaka wa 30 wa wanahisa wa Benki hiyo ambapo unatarajiwa kufanyika Mei,17 huku ukitanguliwa na semina maalum kwa wanahisa ambayo itafanyika Ijumaa Mei 16,2025 katika Ukumbi wa AICC.
Dkt.Laay alisema kuwa benki hiyo imekuwa ikikua siku Hadi siku huku thamani ya hisa katika soko la hisa la dar es salaam likiendelea kukua kwa kasi kutoka shilingi 150 tangu ilipoorodheshwa hadi kufikia shilingi 860 ambapo ni sawa na ukuaji wa asilimia 613.
“Hili ni jambo la kujivunia kwani linaonyesha Imani ya wawekezaji kwa taasisi yetu na udhibiti wa Benki yetu katika kutoa thamani kwa wamiliki wake”Alisisitiza Dkt.Laay
Hata hivyo Mwenyekiti huyo alisema kuwa semina hiyo ya kihistoria itakuwa chini ya kauli mbiu isemayo “Miaka 30 ya Ukuaji Pamoja,na Itafunguliwa rasmi na Makamu wa raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania dkt.Philip Isdory Mpango ambapo ni fursa muhimu ya kutafakari mafanikio Yao,pamoja na changamoto ambazo walizishinda na mwelekeo mpya wa benki hiyo kwa Miaka Ijayo.
Kwa Upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB bw.Abdulmajid Nsekela amesema kuwa benki hiyo imekuwa ikitumia mkutano mkuu wa mwaka wa wanahisa kama fursa ya kujitathmini ili kuendelea kukuza na kuboresha huduma zinazotolewa na benki hiyo.
“Mkutano huo unatuwezesha kukuakutana na wawekezaji walioamini na kuwekeza katika benki Yetu,wanaangalia na kutafakari benki Yao ilipotoka na inapoelekea pamoja na hayo tunatumia kama fursa ya kujitathmini na kujitafakari ili kuweza kufikia maono
Pia Nsekela alisema kuwa maandalizi yote ya mkutano mkuu wa 30 wa wanahisa umekamilika kwa asilimia mia moja.
Benki ya CRDB pia ilizindua Ripoti yake ya mwaka 2024 inayoonesha maendeleo makubwa ya kifedha,kiutendaji,na Kijamii yaliyopatikana katika kipindi hicho.