Na Issa Mwadangala
Wasafirishaji wa abiria kwa kutumia pikipiki (Bodaboda) kijiwe cha Shingo feni kilichopo Kijiji cha Lumbila Wilaya ya Mbozi Mkoani Songwe wametakiwa kuepukana na vitendo vya kujihusisha na mahusiano ya kimapenzi na wanafunzi ikiwa ni pamoja na kufuata na kuzingatia sheria za usalama barabarani ili kuepukana na ajali ambazo zinaweza kusababisha madhara makubwa ikiwemo ulemavu wakudumu.
Kauli hiyo imetolewa Mei 14, 2025 na Polisi kata ya Ruanda Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Happy Lumbe ambapo amewataka wasafirishaji hao kuacha tabia ya kuwa na mahusiano ya kimapenzi na wanafunzi pia wasisite kutoa taarifa za wenzao wenye tabia kama hizo ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa kwa haraka dhidi yao na iwe fundisho kwa jamii.
Kwa kuongezea na kumalizia Mkaguzi Lumbe amewataka wasafirishaji hao kuacha na kuepukana na tabia ya kujichukulia sheria mkononi kwani ni kosa kisheria.