Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Finland Mhe. Alexander Stubb mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 14 Mei, 2025.
Rais wa Jamhuri ya Finland Mhe. Alexander Stubb akikagua Gwaride la heshima lililoandaliwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 14 Mei, 2025.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Finland Mhe. Alexander Stubb wakati wimbo wa Taifa wa Tanzania na ule wa Finland ukiimbwa katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 14 Mei, 2025.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Rais wa Jamhuri ya Finland Mhe. Alexander Stubb, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 14 Mei, 2025.