Na Janeth Raphael MichuziTv -Dodoma
WIZARA ya Madini imehamia rasmi katika ofisi zake za mji wa serikali,huku ikitangaza mikakati rasmi ya utendaji kazi wao,ili kuweza kufikia malengo waliojiwekea hususani kuwaendeleza wachimbaji wadogo.
Mbali na hilo waziri wa wizara hiyo Antony Mavunde amewasisitiza watumishi kuendelea kuchapa kazi kwa bidii ili waweze kutoa huduma stahiki kwa jamii ikiwemo kufikia malengo waliojiwekea.
Mavunde amesema hayo leo jijini Dodoma wakati wizara hiyo ikihamia rasmi katika ofisi zake zilizopo mji wa serikali kwa ajili ya kuendelea na utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku kwa wananchi.
Mavunde amesema,kuhamia kwa watumishi wote wa wizara hiyo katika ofisi moja iliopo mji wa serikali,kutairahisishia jamii kupata huduma zote zinazohusu madini kwa wakati mmoja,ikiwemo kuwapunguzia gharama wananchi wanaojitokeza kutafuta huduma.
Alifafanua zaidi ya kuwa,huduma zote zinazohitajika kwa wananchi zitapatikana katika ofisi za mji wa serikali kitendo ambacho kitawapunguzia gharama watu wanaohitaji huduma katika ofisi za wizara,kutokana na kwamba kila huduma itapatikana eneo moja
“Tunaishukuru Serikali kwa uwekezaji iliofanya katika mji wa serikali wao kama Madini wataendelea kufanya kazi kwa bidii ili kuhakikisha wizara hiyo inafikia malengo iliojiwekea,”alisema Mavunde.
Hata hivyo amesema kuhamia katika ofisi hiyo wametekeleza pia agizo la kamati ya Bunge ya Kudumu ya Nishati na Madini ambayo iliwataka wahamie katika ofisi hizo ili kurahisisha utoaji huduma kwa jamii.
Kutokana na hilo amesema wataendelea kuweka jitihada katika utendaji wao wa kila siku ili kuhakikisha wanafikia malengo hususani katika utendaji kazi wao wa kila siku.
Awali akimkaribisha waziri,Naibu Waziri wa wizara hiyo, Steven Kiruswa ameishkuru Serikali kutokana na uwekezaji iliofanya hadi kufikia mji wa.serikali unakamilika Kwa wizara mbalimbali kuhamia.
Mbali na hilo aliwapongeza watumishi wa wizara hiyo kuendelea kufanya kazi kwa bidii ili kuweza kufikia malengo waliojiwekea katika utendaji kazi wao wa kila siku katika maeneo mbalimbali.
Amesema Wizara hiyo imejipanga kuhakikisha wananchi wake wanapata huduma stahiki zile ambazo watakuwa wanahitaji kuzipata.
Mji huo wa serikali utazinduliwa rasmi kwa utaratibu ambao utapangwa na ofisi ya Waziri mykuu,hivo Wizara mbalimbali zinaendelea kuhamia katika ofisi hizo.